Tuesday , 21 March 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Ujenzi JNHPP wafikia asilimia 82, umeme Juni 2024
Habari Mchanganyiko

Ujenzi JNHPP wafikia asilimia 82, umeme Juni 2024

Bwawa la Umeme Rufiji
Spread the love

MKURUGENZI Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Maharage Chande amesema Ujenzi wa Mradi wa Kuzalisha Umeme wa Julius Nyerere (JNHPP) umefikia asilimia 82 na matarajio ni kuanza kuzalisha umeme Juni 2024. Anaripoti Seleman Msuya, Rufiji …(endelea)

Akizungumza na MwanaHALISI Online leo tarehe 15 Machi 2023, Maharagande amesema tangu Rais Samia Suluhu Hassan aingie maradakani kasi ya ujenzi wa mradi huo imekuwa ikiienda kasi kutoka asilimia 36 mwaka 2021 hadi 82, 2023.

Amesema mradi huo ambao unatarajia kuzalisha umeme megawati 2,115 unategemea maji kutoka Bwawa la Mwalimu Nyerere ambapo hadi sasa maji yamejaa kwa mita 134 kutoka usawa wa bahari, ambapo Desemba 22, 2022 Rais Samia aliruhusu maji kujaa.

Mkurugenzi huyo amesema kwa sasa wakandarasi wanaendelea kufunga mitambo wa kwanza wa kuzalisha umeme, hivyo matarajio yao ni kwamba hadi kufika Juni 2024 mitambo yote tisa itakuwa imefungwa na kuzalisha umeme.

“Ujenzi wa Mradi wa JNHPP umefikia asilimia 82, maji yameaa kwa mita 134 kutoka usawa wa bahari na matarajio yetu ni mradi huu uanze kuzalisha umeme Juni 2024 kama hakutakuwa na changamoto,” amesema.

Mkurugenzi huyo amesema kwa sasa hawawezi kusema tarehe rasmi ya uzalishaji umeme na hawataki kuisema kwa kuwa haipo, hivyo kuwataka Watanzania kuwa na subira kwani ujenzi unaenda vizuri.

Amesema mradi huo wa aina yake ili kukamilika unahitaji kuangalia masuala ya mazingira, vituo vya kupooza na usafirishaji ambayo ni muhimu katika miradi.

Maharage amesema kwa sasa wanaendelea kupima kazi, huku mitambo ikiendelea kufungwa na kwamba watatoa taarifa kwa kila hatua ambayo itafikiwa.

Aidha, mkurugenzi huyo amesema katika kuhakikisha mradi huo unakuwa endelevu Bodi ya TANESCO imefanya maamuzi kwamba wawekeze katika masuala ya mazingira kwa kushirikiana na wadau wote.

Alisema pia wamejadiliana, kukubaliana na mpango kazi na bodi za maji za mabonde, ili kuhakikisha vyanzo vya maji vinatunzwa ili maji yawe yanatiririka muda wote.

Mkurugenzi huyo alisema shirika hilo limejipanga kuhakikisha huduma ya nishati ya umeme inapatikana kwa uhakika katika maeneo yote, hali ambayo itachochea ukuaji wa uchumi na huduma za jamii.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Maji Bonde la Rufiji (RBWB), Mhandisi Florence Mahay, alisema bodi hiyo inaendelea kutunza vyanzo vya maji vinazunguka bonde, ili kuwepo na maji ya uhakika kwenye Bwawa la Mwalimu Nyerere

Amesema iwapo mvua zitanyesha kwa kipindi cha miaka miwili ya msimu, Bwawa la Mwalimu Nyerere litakalozalisha megawati 2,115 za umeme litakuwa limejaa maji.

1 Comment

  • Ahsante kwa hatua hii. Utunzaji wa vyanzo vya maji uende sambamba na ujazaji wa bwawa msimu wa masika na muwe na ziada ya ujazo ukame ukitokea. Bila mikakati mtatia aibu kwa kushindwa kuwa na plani B.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Tanzania yakabidhi rasmi msaada nchini Malawi

Spread the loveWAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,...

Habari Mchanganyiko

Bashe: Tumeshagawa pikipiki 5,500 kati ya 7,000 kwa maafisa ugani

Spread the love  WAZIRI wa Kilimo, Hussen Bashe, amesema wizara hiyo tayari...

Habari Mchanganyiko

Spika Tulia awapa neno mawaziri utekelezaji mashamba ya pamoja

Spread the love  SPIKA wa Bunge, Dk. Tulia Ackson, amewataka mawaziri kushirikiana...

Habari Mchanganyiko

Ukosefu wa maadili kwa wakunga, wauguzi bado changamoto

Spread the loveIMEELEZWA kuwa vitendo vya uvunjifu wa maadili kwa  wauguzi na...

error: Content is protected !!