Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Ujenzi Ikulu ya Chamwino kukamilika Mei 2022
Habari za Siasa

Ujenzi Ikulu ya Chamwino kukamilika Mei 2022

Jengo la Ikulu ya Chamwino Dodoma
Spread the love

 

UJENZI wa Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma nchini Tanzania umefikia asilimia 91 na utakamilika Mei 2022. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Hayo yamesemwa jana Jumapili, tarehe 16 Januari 2022 na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Mhandisi Daudi Kondoro aliyesema, ujenzi huo utakamilika na kukabidhiwa Mei kama inavyotarajiwa kwani sasa uko katika hatua za mwisho za ukamilishaji.

Mhandisi Kandoro alikuwa akitoa maelezo kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ambaye alikagua ujenzi huo na kuonesha kuridhishwa na kasi ya ujenzi na ubora wa majengo hayo huku akimtaka mkandarasi ahakikishe mradi huo unakamilika Mei 2022.

Majaliwa alisisitiza wakandarasi kuhakikisha wanakamilisha mradi huo kwa wakati na kuwapongeza wote wanaohusika na ujenzi.

“Tunataka kumuwezesha Mheshimiwa Rais kufanya kazi katika eneo lake maalum na afanye kazi katika mazingira mazuri na kwa ufanisi,” alisema Majaliwa.

“Nimefurahishwa na taarifa kwamba ujenzi huu umefikia asilimia 91 na hatua iliyobaki hizi asilimia tisa ni kazi ndogondogo kama uwekaji wa milango, njia za mifumo ya hewa na umeme na zote zinaenda vizuri.”

Waziri Mkuu alisema Rais Samia Suluhu Hassan pia anatarajia kuona ujenzi huo unakamilika kwa wakati.

Waziri Mkuu alilipongeza Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwa kutekeleza ujenzi huo kwa ufanisi. “Ramani iliyoko hapa iko sawasawa na jengo la Ikulu lililoko Dar es Salaam, Wakandarasi wetu mmefanya kazi kubwa sana, Hii imedhihirisha kuwa nchi yetu ina wataalam wa kutosha kujenga aina yoyote ya majengo.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!