September 29, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Uhuru wa habari wamtesa Nape, CCM

Spread the love

[dropcap][/dropcap]

UHURU wa kujieleza, kujadili na kuhoji mambo kwa upana wake ndani ya mipaka ya Tanzania, ndio unaomtesa Nape Nnauye, Wazari wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, anaandika Pendo Omary.

Mageuzi ya kupata habari yanayoonekana kutekenya bongo za wananchi, yamekuwa mwiba mkali kwa Nape na Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) hivyo kuminya uhuru huo kwa kutumia mamlaka walizonazo.

Baada ya Nape kufungia kwa Gazeti la MAWIO, Mseto kwa kutumia sheria kandamizi, sasa amevifungia vituo viwili vya redio nchini kwa muda usiojulikana.

Vituo hivyo ni Redio Five ya jijini Arusha na Redio Magic Fm ya jijini Dar es Salaam kwa kile alichokiita kurusha ‘vipindi vyenye uchochezi.’

Kituo cha utangazaji cha Redio Five kinadaiwa kumilikiwa na Edward Lowassa, Waziri Mkuu Mstaafu ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Lowassa urais katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana kupitia Chadema na kuungwa mkono na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

Hatua ya Lowassa kugombea urais kupitia Chadema ilitokana na jina lake kukatwa na Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika mchakato wa kumpata mgombea wa urais kupitia chama hicho.

Nape amesema, amejiridhisha kuwa Redio 5 katika kipindi cha matukio kilichorushwa tarehe 25 Agosti, 2016 saa 2.00 – 3.00 usiku ambapo katika kipindi hicho cha mahojiano, mgeni alikuwa Godbless Lema, Mbunge wa Arusha Majini, maneno ya uchochezi yalitoa.

Amesema, licha ya mbunge huyo kutoa lugha hizo, watangazaji wa kipindi hicho walishindwa kumsahihisha jambo analodai, linakwenda kinyume na sheria ya utangazaji.

Amedai, mnamo tarehe 17 Agosti 2016 katika kipindi cha Morning Magic kilichorushwa saa 1.00 asubuhi – saa 2.30 katika kipengele cha Kupanga Rangi, watangazaji wa kipindi hicho walisikika wakitoa maneno anayoeleza kuwa ni ya uchochezi.

“Watangazaji hawa wa Magic walisema, kama Rais anavunja Katiba sasa wananchi wa chini wafanyaje, nao lazima watafanya hivyo,” amesema Nape.

Amesema, baada ya kuvifungia vituo hivyo kwa muda, ameitaka Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kukutana ili wapitie pande zote mbili za redio hizo ili waweze kujitetea.

Amesema, kamati hiyo ikishakutana na kusikiliza utetezi wa redio hizo, basi yeye atachukua hatua ya kuvifungulia au kuendelea kuvifungia.

Kufungiwa mfululizo kwa vituo hivyo ni mwendelezo wa rekodi anazojiwekea Nape kufungia vyombo vya habari vingi kwa muda mfupi.

error: Content is protected !!