Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Uhuru wa Habari: Tanzania yazidi kuporomoka
Habari Mchanganyiko

Uhuru wa Habari: Tanzania yazidi kuporomoka

Mwenyekiti wa TEF, Deodatus Balile
Spread the love

UHURU wa vyombo vya Habari nchini Tanzania, umekuwa ukiporomoka mwaka hadi mwaka kwa majibu wa taarifa ya waandishi wa habari wasio na mipaka dunia. Anaripoti Mwandishi Wetu, Arusha…(endelea).

Mpaka mwaka 2020, Tanzania imeanguka mpaka nafasi ya 123. Mwaka 2016 ilishika nafasi ya 71 kati ya nchi 180, mwaka 2017 iliporomoka mpaka nafasi ya 83, mwaka 2018 ikaanguka ten ana kushika nafasi ya 93.

Takwimu hizo zimeelezwa na Deodatus Balile, Kaimu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), leo tarehe 3 Mei 2021 katika kilele cha Maadhimisho ya Uhuru wa Habari Duniani. Maadhimisho hayo yamefanyika jijini Arusha.

Akisoma taarifa hiyo, Balile amesema, mpaka mwaka 2021 Tanzania imeporomoka kwa nafasi 53 ikilinganishwa na nafasi iliyokuwa nayo mwaka 2016.

Kwenye maadhimisho hayo, Balile amesema taarifa hio ni mbaya kwa Taifa huku akiiomba serikali kufanya liwezekanalo ili kubadilisha mazingira hayo.

“”Tunaomba hali ya uhuru wa habari iboreshwe nchini,”amesema Balile huku akitoa wito kwa taasisi na wadau wa habari kuwa na mjadala wa kitaifa.

Katika maadhimisho hayo, Innocent Bashungwa, Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, amedai hali ya vyombo vya Habari nchini haipo kama ilivyoelezwa.

Amesisitiza, kwamba kutokana na uhuru wa habari nchini, serikali imesajili magazeti 246, runinga 53, redio 194, redio za mtandao 23, blogs 120 na runinga za mtandaoni 440.

Bashungwa amesisitiza, serikali inafanya kazi kubwa kuimarisha uhuru wa habari nchini.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga kuongoza usambazaji wa mitungi ya gesi 10,000 ya Taifa Gas

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ameahidi kuongoza kwa ufanisi...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyabiashara, wawekezaji China waridhia kuwekeza bil. 800 katika sekta 5 nchini

Spread the loveUJUMBE wa wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa kutoka Jimbo la Changzhou...

Habari Mchanganyiko

Bil. 4.42 kumaliza uhaba maji kata 2 Musoma Vijijini

Spread the loveWANANCHI wa kata za Busambara na Kiriba, Jimbo la Musoma...

error: Content is protected !!