
Rais Uhuru Kenyatta
Rais wa Kenya Uhuru Kenyata amezitaka nchi za Afrika kuacha kutegemea misaada ya nchi za nje, akiamini kuwa misaada hiyo sio msingi wa maendeleo.
“Utegemezi unaodhaniwa kuwa ni fadhila nilazima ukome” Uhuru aliyasema haya kwenye twita yake siku chache kabla ya kuhudhuria mkutano wa Umoja wa Nchi za Afrika utakaokutanisha takribani marais 50 kutoka nchi mbalimbali za Afrika zilizopo kwenye umoja huo.
Kenya inaaminika kuwa nitegemezi kwa misaada ya nje kwenye bajeti yake kwa kiwango cha asilimia 5-6, wakati Tanzania nitegemezi kwa takribani asilimia 30 kwenye bajeti ya Taifa.
More Stories
Marekani yafanya ‘uchochezi,’ yawaonya wanaokuja Tanzania
Balozi aliyeuawa Congo, mwili warejeshwa Roma
Tiger Wood apata ajali mbaya, alazwa ICU