August 9, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Uhujumu uchumi: Vigogo wafurika kwa DPP

Picha ndogo ni miongoni mwa watuhumiwa waliopo kwenye magareza mbalimbali nchini mpaka sasa kwa kesi za uhujumu. Picha kubwa ni Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Biswalo Mganga.

Spread the love

IDADI ya barua za kuomba msamaha kutoka kwa watuhumiwa wa uhujumi uchumi, zinaingia kwa kasi katika ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP). Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).  

Taarifa zaidi zinaleleza, washtakiwa kutoka magereza mbalimbali wameanza kutekeleza masharti ya Biswalo Mganga (DPP), ya kuandika barua zao kupitia wakuu wa magereza na kisha kufikishwa ofisini kwake.

Miongoni mwa watuhumiwa waliopo kwenye magareza mbalimbali nchini mpaka sasa na wanaotuhumiwa kwa mashitaka hao, ni hao waliopo pichani.

Uthibitisho wa kasi ya uandikaji barua kwenda kwa DPP, unaelezwa na Balozi Augustine Mahiga, Waziri wa Katiba na Sheria ambaye anasema, “wameanza kufanya hivyo kwa kasi katika ofisi ya DPP.”

Jumapili ya tarehe 22 Septemba 2019, Rais John Magufuli alishauri ofisi ya DPP, kwamba wale wenye kesi za uhujumu uchumi na utakatishaji fedha, kama wapo tayari kuomba radhi na kurejesha fedha, ofisi hiyo iangalie utaratibu wa kuwaachia ndani ya siku saba.

Dk. Mahiga amewaambia Watanzania wakati akiwa kwenye mahojiano na kituo cha Televisheni cha Azam tarehe 24 Septemba 2019, kwamba kauli ya Rais Magufuli imeanza kufanyiwa kazi na wenye tuhuma hizo.

“Hapo mapema nilizungumza na DPP,” amesema Dk. Mahiga na kuongeza “maombi ya msamaha yanaingia kwa kasi sana lakini hata hivyo wanapaswa kuyachunguza. Kazi hiyo itafanywa kwa kushirikiana na idara ya usalama.”

Kwenye mjadala huo, alikuwepo DPP ambaye alisema, watuhumiwa wana uhuru wa kuamua “kama watuhumi wataamua kuendelea kukaa huko, tutaendelea kukaa naye.”

Tangua Rais Magufuli kuingia madarakani mwaka 2015, baadhi ya wafanyabiashara, wanasiasa na waandishi wamekuwa wakikamatwa na kupandishwa kizimbani kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo uhujumu uchumi na utakatishaji fedha.

Miongoni mwa waliofikishwa mahakamani kwa tuhuma hizo ni pamoja na mfanyabiashara James Rugemarila na Harbinder Singh Sethi, mmiliki wa kampuni ya kufua umeme ya IPTL.

Wote wanakabiliwa na mashtaka 12 ikiwa ni pamoja na la utakatisha fedha na kuisababisha serikali hasara ya Dola za Marekani 22, 198,544.60 na Sh 309, 461,300158.27. kwa mara ya kwanza walifikishwa mahakamani tarehe 19 Juni 19 2017.

Mkurugenzi wa Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka Dar es Salaam (Udart), Robert Kisena, mke wake Florencia Mshauri na wenzao watatu wanakabiliwa na tuhuma za uhujumu uchumi.

Kulthum Mansoor, aliyekuwa Mkurugenzi wa Mipango, Ufuatiliaji na Tathimini wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), anakabiliwa na mashtaka manane ya kughushi, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na kutakatisha Sh. 1.477 Bil.

Evance Aveva, aliyekuwa Rais wa Klabu ya Simba na Godfrey Nyange (Kaburu), Makamu wake licha ya kuondolewa shtaka la kutakatisha fedha, wameendelewa kushikiiliwa baada ya DPP kupinga kuondolewa kwa mashtaka ya kutakatisha fedha.

Harry Kitilya, aliyekuwa Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) pamoja na wenzake Sioi Solomon, Shose Sinare, Alfred Misana na Bedason Shallanda wanakabiliwa na mashtaka 58 ikiwemo uhujumu uchumi.

Waliokuwa viongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamali Malinzi (Rais), Celestine Mwesigwa (Katibu Mkuu) na Nsiande Mwanga (Mhasibu) wanakabiliwa na mashtaka 20 yakiwemo ya utakatishaji fedha.

error: Content is protected !!