Monday , 29 May 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Uhujumu uchumi: Kigogo mwingine ajitosa kwa DPP
Habari za Siasa

Uhujumu uchumi: Kigogo mwingine ajitosa kwa DPP

Kuluthum Mansoor, akiwa mahakamani wakati wa kesi yake
Spread the love

KULUTHUM Mansoor, aliyekuwa Mkurugenzi wa Mipango, Ufuatiliaji na Tathimini wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), amekiri kosa na kutaka yaishe. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Elia Mwingira, Wakili wa Utetezi ameiambia Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kwamba wameandika barua kwenda kwa Mkurugenzi wa Makosa nchini (DPP) Biswalo Mganga kukiri makosa ya Kuluthum.

Kigogo huyo wa Takukuru anakabiliwa na mashtaka manane likiwemo la utakatishaji fedha kiasi cha Sh. 477 Bil. Mashitaka mengine ni kughushi, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Wakili wa Kuluthum ametoa kauli hiyo baada ya Wankyo Simon, wakili wa serikali mwandamizi kudai mahakamani hapo kuwa, upelelezi haujakamilika.

Hata hivyo, wakili Mwingira ameiomba mahakama kuzingatia kwamba, mteja wake tayari ameandika barua hiyo kwa lengo la kutaka apatiwe haki yake ya msingi.

Pamoja na maelezo hayo, Hakimu Mfawidhi, Kelvin Mhina ameahirisha shauri hilo mpaka tarehe 16 Oktoba 2019 itakapotajwa tena.

Jumapili ya tarehe 22 Septemba 2019, Rais John Magufuli alishauri ofisi ya DPP, kwamba wale wenye kesi za uhujumu uchumi na utakatishaji fedha, kama wapo tayari kuomba radhi na kurejesha fedha, ofisi hiyo iangalie utaratibu wa kuwaachia ndani ya siku saba.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Uamuzi juu ya wakurugenzi kusimamia uchaguzi 13 Juni

Spread the love  MAHAKAMA ya Afrika ya Haki za Binadamu (ACHPR), imepanga...

Habari za Siasa

Musoma Vijijini waomba ujenzi wa barabara uanze haraka

Spread the loveJIMBO la Musoma Vijijini, mkoani Mara, limeomba Serikali kuhakikisha ujenzi...

Habari za Siasa

ACT Wazalendo yaanika madudu miradi ya ujenzi, moundombinu

Spread the loveCHAMA cha ACT Wazalendo kimeeleza wasiwasi juu ya uelekeo wa...

Habari za Siasa

Samia ashuhudia utiaji saini ujenzi wa minara 758 ya bilioni 265

Spread the love  RAIS Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa kampuni za...

error: Content is protected !!