May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Uhondo wa Ligi Kuu Bara kurejea kesho

Spread the love

 

LIGI Kuu Tanzania Bara inarejea tena kesho kwa kupigwa michezo miwili, ambapo Simba itakuwa Ugenini kuikabili Dodoma Jiji FC kwenye Uwanja wa Jamhuri, huku KMC FC itawaalika Namungo FC kwenye Uwanja wa Uhuru, Jijini Dar es Salaam. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Ligi hiyo ilisimama mwezi mmoja kupisha michuano ya Kombe la Mapinduzi pamoja na michuano ya Kombe la Mataifa Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN) ambayo Tanzania walikuwa washiriki.

Michezo hiyo ya siku ya kesho tarehe 4 Februari 2021, kwa timu ambazo zilikuwa na michezo mkononi (viporo) Simba na Namungo kutokana na ushiriki wao kwenye michuano ya kimataifa.

Michezo mingine ya viporo itachezwa tena tarehe 7 Februari 2021, ambapo Simba watakuwa kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa kuikaribisha Azam FC, huku Namungo wakiwa uwanja wa nyumbani kuwaalika Ruvu Shooting.

Mpaka Ligi hiyo inasimama Yanga walikuwa kileleni kwenye msimamo wakiwa na pointi 44 baada ya kucheza michezo 18, huku nafasi ya pili ikishikwa na Simba yenye pointi 35, wakiwa wamecheza mechi 15.

error: Content is protected !!