March 1, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Uhamiaji yajiandaa kutoa elimu kwa jamii

Mji wa Dodoma

Spread the love

IDARA ya uhamiaji mkoa wa Dodoma imeandaa mpango maalum wa kuwafikia wananchi kuanzia ngazi ya kitongoji hadi wilaya kwa lengo la kutoa elimu ya utambuzi wa wahamiaji haramu, anaanadika Dany Tibason.

Aidha, kutokana na Dodoma kuwa makao makuu ya nchi wameanza kuimarisha ulinzi na msako kwa ajili ya kufichua watu ambao wanaingia nchi kinyume cha sheria.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Dodoma, Peter Kundy, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kumalizika kwa mazoezi ya viungo yaliyofanyika katika uwanja wa mpira wa Jamhuri mjini hapa.

Kundy amesema kwa kuwa Dodoma ni makao makuu ya nchi zipo changamoto nyingi za watu wengine kutoka nje ya nchi kwa lengo la kutaka kutumia fursa za kujipatia kipato.

error: Content is protected !!