August 15, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Uhamiaji wakamata 102 Dar

Spread the love

IDARA ya Uhamiaji jijini Dar es Salaam imekamata wahamiaji haramu 102 walioingia na kuishi nchini bila vibali halali vya serikali, anaandika Happiness Lidwino.

Pia, idara hiyo imewakamata Watanzania watatu wanaodaiwa kuhusika kuwahifadhi wahamiaji hao pamoja na kuzuia maofisa uhamiaji kutimiza majukumu yao.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini humo, John Msumule, Kamishna wa Idara ya Uhamiaji Mkoani Dar es Salaam amesema, wahamiaji wamekamatwa baada ya idara hiyo kufanya msako mkali ambao ulianza tangu mwanzoni mwa mwezi huu na kufanikiwa kuwakamata wahamiajia hao.

Amesema, wahamiaji ambao wengi wao wametoka nchi za India pamoja na Nepal walikamatwa kwenye kampuni moja iliyopo Mikocheni wilayani Kinondoni ambapo amedai, baada ya kuwakamata na kuwahoji, walibainika wamefika jijini humo kwa shughuli za kucheza mziki.

Msumule ameeleza kuwa, mara baada ya maofisa hao kutaka waoneshwe vibali cha kuingia nchini, wahamiaji hao walionesha vibali ambavyo vilionesha muda wa kuishi nchini umekwisha.

Hata hivyo Kamishna Msumule amesema, idara yake inawashikilia Watanzania ambao walihusika katika kuwahifadhi wamiaji hao kwa lengo la kuwaficha ili mamlaka husika zishindwe kuwakamata pamoja na kuwatafutia nyaraka zitakazowawezesha kuishi nchini.

Amesema, wahamiaji hao pamoja na watanzania hao,watafikishwa Mahakamani mara baada ya uchunguzi kukamilika.

Sanjari na hayo, Kamishna Msumule amesema idara yake inakumbana na changamoto ambazo amedai zinachangia kushindwa kufanya kazi kikamilifu za kupambana na wahamiaji hao.

Amezitaja changomoto hizo kuwa ni, ukosefu wa magari amabyo watayatumia kufanya doria,pamoja uhaba wa rasilimali watu,hivyo ameiomba Serikali kutatua changomoto hizo ili Idara hiyo iweze kupambana na wahamiajia haramu.

error: Content is protected !!