Sunday , 29 January 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Uhakiki laini za simu mwisho 13 Februari, 2023
Habari Mchanganyiko

Uhakiki laini za simu mwisho 13 Februari, 2023

Spread the love

 

SERIKALI imeongeza siku 14 kwa Watanzania waliosajili laini zao za simu kuhakiki laini hizo kabla ya kufikia tarehe 13 Februari, 2023 saa 10 jioni ambapo laini zote ambazo hazijahakikiwa zitazimwa. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Hatua hiyo imekuja baada ya kuibuka wimbi la matapeli wanaotumia laini zilizosajiliwa kutapeli watu na wengine kufanya matukio ya kihalifu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 24 Januari, 2023 jijini Dodoma Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema sekta ya mawasiliano inakua na mpaka zipo laini za simu zinatotumika zaidi ya milioni 60.

Amesema hadi kwa mujibu wa takwimu za Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) hadi kufikia tareh 19 Januari, 2023 laini milioni mbili zilikuwa hazijahakikiwa.

“Serikali kupitia TCRA tulichukua hatua za kufanya usajili wa laini za simu kwa kutumia biometric – alama za vidole na vitambulisho vingine ambapo dirisha lilifungwa tarehe Mei, 2019 na lilifungwa Disemba 2021.

“Tulianzisha kampeni ya kuhakiki laini hizo na hadi sasa zoezi linaendelea kwani mwanzoni ilikuwa tuende hadi mahali lakini tukaongeza muda mara mbili na ya tatu ambayo ilikuwa ya mwisho ni tarehe 31 Januari, 2023.

Nape Nnauye, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Tekinolojia

Amesema kwa kuwa kuna laini nyingi mtaani ambazo watu wametumia vitambulishi vya watu wengine kusajili, sasa zitaenda kuzimwa hivyo wanatakiwa kuhakiki laini hizo ili kutokomeza utapeli wa ‘ile pesa tuma kwa namna hii’ .

“Tunaenda kuzima ambazo zimesajiliwa lakini zimesajili kwa uongo, kama huzijasajiliwa kwa uongo nenda kaihakiki laini yako, yeyote aliyesajili kwa uongo hawezi kuihakiki kwa sababu mfumo utamuumbua, hivyo tumeongeza siku 14.

“Mpaka tarehe 13 Februari siku moja kabla ya siku ya wapendanao tunataka anga la mawasiliano liwe salama, iwe siku ya furaha.. watu wakae wakiwa salama,” amesema Nape.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Huawei Tanzania yatajwa miongoni mwa waajiri bora kimataifa

Spread the loveKAMPUNI ya Huawei Tanzania imetajwa kuwa mwajiri bora nchini na...

Habari Mchanganyiko

Waziri wa uchumi wa Finland atua nchini, kuteta na mawaziri 7

Spread the loveWAZIRI wa Masuala ya Uchumi wa Finland, Mika Tapani Lintilä...

Habari Mchanganyiko

Asimilia 79 wafeli somo la hesabu matokeo kidato cha nne

Spread the loveWATAHINIWA wa shule 415,844 sawa na asilimia 79.92 ya watahiniwa...

Habari Mchanganyiko

NECTA yafuta matokeo ya watahiniwa 333 kwa kuandika matusi, kudanganya, 286 yazuiwa

Spread the loveBARAZA la Mitihani la Tanzania (Necta) leo Jumapili limetangaza kuyafuta...

error: Content is protected !!