June 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Uhai Mgodi Mchuchuma ni miaka 100

Mtambo wa kupima kiasi cha madini yaliyomo kwenye mgodi wa Mchuchuma

Spread the love

SERIKALI imesema, uhai wa Mgodi wa Mchuchuma unakadiriwa kuwa ni miaka 100 wakati mgodi wa Liganga ni miaka 50. Anaandika Dany Tibason … (endelea).

Taarifa hiyo ilitolewa bungeni jana na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Rita Kabati (CCM).

Katika swali lake Kabati alitaka kujua serikali imefikia wapi katika mkakati wake wa kuvuna rasilimali ya chuma hususan katika migodi ya Liganga na Mchuchuma ili kuendeleza viwanda vya chuma nchini na kuleta mabadiliko ya viwanda nchini.

Amesema, kutokana na migodi hiyo kuwa na ukomo wa uhai, lazima Serikali ichukue tahadhari za kutosha kabla ya kuanza  kuchimba katika migodi hiyo ili mradi utakapoanza uwanufaishe Watanzania wote.

“Serikali imeipatia  Kampuni ya China International Resources Limited (TCIMRL) leseni ya uchimbaji mkubwa wa madini ya chuma katika eneo la Liganga leseni ambayo nifakia ukomo wake mwaka 2029,” amesema Kitwanga.

Amesema, Kampuni hiyo ya TCIMRL ni kampuni ya ubia kati ya Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) inayomiliki asilimia 20.

Naibu Waziri amesema, Kampuni ya TCIMRL inaendelea na maandalizi ya kufungua mgodi wa chuma kwenye leseni ya Liganga sambamba na uanzishwaji wa kiwanda cha kutengeneza chuma Liganga na mgodi wa Makaa ya Mawe katika eneo la Mchuchuma.

Kwa mujibu wa Kitwanga, miradi hiyo ya Mchuchuma na Liganga inategemewa sana kwani itakapokamilika italeta manufaa kwa utoaji wa ajira kwa Watanzania wapatao 3,049 na kuchangia mapato yatokanayo na mrabaha na kodi mbalimbali.

Kitwanga amesema, manufaa mengine yasiyokuwa ya moja kwa moja yanakadiriwa kufikia Dola za Marekani 1,034 Milioni.

error: Content is protected !!