Friday , 19 April 2024
Home Kitengo Maisha Afya Uhaba wa vitanda watesa wachangia damu
Afya

Uhaba wa vitanda watesa wachangia damu

Baadhi ya wakazi wa Dar es Salaam wakichangia damu
Spread the love

MPANGO wa Damu Salama, unakabiliwa na uhaba wa vitanda kwa vinavyotumiwa na watu wanaofika hapo kwa ajili ya kuchangia damu kwa hiari, anaandika Nasra Abdallah.

Mratibu wa Huduma za Maabara Wilaya ya Ilala wa Mpango wa Damu Salama, Petrobasi Hassan ameyasema hayo wakati wa vijana wa Kanisa la Assemblies of God (TAG) Wilaya ya Tabata, Jimbo la Mashariki ya Kati, walipokwenda kuchangia damu.

Waumini hao walijitolea damu kwa hiari ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku ya vijana wa Kanisa hilo.

Hassan amesema mahitaji halisi ni kuwa na vitanda 15, lakini walivyonavyo kwa sasa ni vinne jambo ambalo linawafanya wachukue muda mrefu kumhudumia mtu mmoja.

Kutokana na tatizo hilo aliwaomba wahisani mbalimbali watakaoguswa kuwasaidia vitanda ili waweze kurahisha kazi yao katika suala zima la ukusanyaji damu kutoka makundi mbalimbali ya jamii.

Mbali na msaada wa vitanda pia amesema kuna uhitaji wa soda na maji na glucose ambavyo vyote hivi hutumika kuwapa watu wanaokwenda kutoa damu katika maeneo mbalimbali.

Mkurugenzi wa Idara ya Vijana Tabata(CA’S), Felix Kulaya, amesema moja ya jambo lililowasukuma kuchangia damu ni kuwa moyo wa kutaka kusaidia kuokoa maisha ya watu.

“Tumekuwa tukisikia taarifa kutoka kwa wataalam mbalimbalk kuwa wakina mama wajawazito, watoto na wale wanaopata ajali wamekuwa wakipoteza maisha kutokana na kukosa damu jambo ambalo limewagusa vijana na kuamua kuchangia damu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari za Siasa

Serikali yasaka watumishi afya ngazi ya jamii 8,900

Spread the loveSERIKALI imeanza utekelezaji wa mpango jumuishi wa wahudumu wa afya...

AfyaHabari za SiasaTangulizi

Bima ya afya kwa wote kuanza Aprili, wajane kicheko

Spread the loveSHERIA ya Bima ya Afya kwa Wote, inatarajiwa kuanza kutumika...

AfyaHabari Mchanganyiko

Marekani kuipa Tanzania bilioni 980 kudhibiti VVU, UKIMWI

Spread the loveSERIKALI ya Tanzania inatarajiwa kupewa msaada wa fedha kiasi cha...

AfyaHabari Mchanganyiko

Wanavijiji wajenga zahanati kukwepa umbali mrefu kupata huduma

Spread the loveWANAVIJIJI wa Kata ya  Musanja Jimbo la Musoma Vijijini, mkoani...

error: Content is protected !!