January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Uhaba wa maji waikabili Chamwino

Msichana akichota maji kwa kutumia mkokoteni wa Punda

Spread the love

WANANCHI wa wilaya ya chamwino katika jimbo la Chilonwa wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa maji jambo ambalo linatishia usalama wa afya zao. Anaandika Dany Tibason, Dodoma … (endelea). 

Mbali na kutishia usalama wa afya zao, wananchi hao wanatumia muda mwingi kutafuta maji jambo ambalo linasabisha kukwama kwa shughuli za maendeleo pamoja na baadhi ya wanafunzi kushindwa kwenda shuleni.

Kauli hiyo ilitolewa na wakili wa kujitegemea John Chigongo na mtangaza nia ya kuwania ubunge katika jimbo la Chilonwa kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) alipokuwa akizungumza na wananchi wa Chinangali “ A” katika mkutano wa hadhara.

Wakili Chigongo alisema licha ya Jimbo hilo kuongozwa na viongozi kutoka CCM lakini wananchi wa Chilonwa ni kama wametelekezwa kutokana na na kukosekana kwa huduma muhimu.

Amesema  wananchi wa chilonwa kwa ujumla wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na ukosefu wa huduma za afya, huduni wa elimu pamoja na ukosefu wa miundombinu ya kielimu.

Mtangaza nia huyo aliwataka wananchi wa jimbo hilo kuhakikisha wanafanya mabadiliko ya kweli ili kuiondoa CCM madarakani kwani chama hicho kimesababisha watanzania wengi kuwa masikini.

“Mimi ni mwanasheria ninajua wazi Tanzania siyo masikini umasikini ambao unatusumbua sisi watanzania hautokani na mpango wamungu bali unatokana na utawala mbovu wa serikali inayoongozwa na CCM” amesema.

Nae Mwenyekiti wa Baraza la  vijana Chadema Mkoa wa Dodoma,(BAVICHA) Manyanya  Manyanya, aliwataka vijana kukubali mabadiliko ili kujiletea maendeleo.

Manyanya amesema  ni wakati muafaka vijana kuonesha ujasiri wao katika kudai mageuzi ambayo yatakuwa mkombozi kwao ili kuondokana na mwimba wa umasikini ambao ni CCM.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Oganaizeisheni na mafunzo (Chadema), taifa na msimamizi wa kanda, Benson Kigaila alisema umasikini kwa watanzania hauwezi kuisha kama hakutakuwepo na mabadiliko ya kweli hasakuiondoa CCM madarakani.

Akihutumia umati wa wananchi wa Wilaya ya Chamwino katika jimbo la Chamwino Mkoani hapa amesema  utawala uliopo madarakani kwa kupitia CCM unafanya makusudi wananchi waendelee kuwa masikini ili waweze kutawaliwa kirahisi.

Kigaila amesema  wapo viongozi wengi ndani ya serikali ya CCM ambao wanajichotea fedha kwa malengo ya kujinufaisha na wezi hao wanalindana.

“Wananchi mmesikia wapo watu wamejichotea mabilioni ya fedha katika akaunti ya Tegeta Escor na wengine kwa dharau kabisa wanasema ni hela ya mboga lakini hakuna hatua yoyote ambayo watu hao wamechukuliwa.

“Lakini angalia ndani ya miaka 55 ya Uhuru wananchi wa Chinagali hamna maji safi na salama hadi inafikia undoa zinapata misukosuko,wanafunzi wanashindwa kuhudhuria mafunzo kwa wakati lakini mbayazaidi ni pale ambapo hata kiafya maji mnayotumia yanatishia amani” amesema  Kigaila.

error: Content is protected !!