January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Uhaba wa damu waikumba hospitali Dodoma

Spread the love

BAADHI waganga katika hospitali za wilaya mkoani Dodoma, wamelalamikia ukosefu wa damu salama katika hospitali zao, jambo ambalo linasababisha usumbufu mkubwa kwa wagonjwa. Anaandika Dany Tibason, Dodoma … (endelea).

Mmoja wa waganga katika moja ya hospitali hizo za wilaya ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini kwa madai kuwa siyo msemaji, amesema tatizo hilo limekuwa sugu licha ya kuwa serikali kulitambua huku ikilifumbia macho.

Amesema shida kubwa zaidi inajitokeza wakati wa kuwa hudumia wagonjwa ambao wanahitaji damu hususani akina mama wajawazito, watoto chini ya miaka mitano, waliopata ajali pamoja na wale ambao wanafanyiwa upasuaji.

Katika hatua nyingine waganga hao walisema kuwa ukosefu mkubwa wa damu salama unatokana na serikali kushindwa kulipa uzito suala hilo na kusababisha wagonjwa kuwalalamikia waganga na wauguzi katika hospitali hizo.

Hata hivyo, wamesema ukosekana kwa fedha, ndiyo chanzo kikubwa kinachokwamisha upatikanaji wa damu salama kwa ajili ya kutafuta katika maeneo mbalimbali.

Aidha, Waganga hao wamesema damu nyingi inapatikana kutokana na wanafunzi ambao kama wangetembelewa zaidi damu ingeweza kupatikana kwa urahjisi zaidi.

Baada ya kupokea malalamiko kwa waganga wa hospitali za wilaya, MwanaHALISI Online, ililazimika kutembelea katika shule mbalimbali za sekomndari kwa ajili ya kutaka kujua kama wanafunzi hao wapo tayari kutoa damu.

Wananfunzi ambao waliweza kuzungumza wamesema wao wapo tayari kujitolea damu lakini kwa sasa idara ya kitengo cha damu salama hakiwatembelei wanafunzi hao.

Mmoja wa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Jamhuri Asha Salum, amesema yeye ni mmoja wapo wa wanafunzi ambaye yupo tayari kujitolea kutoa damu lakini wale ambao wanatakiwa kufika shuleni hapo kwa ajili ya kutoa damu hawatembelei shule hizo.

Naye Daudi John, amesema anasikitishwa sana na baadhi ya wagonjwa kupoteza maisha kwa ajili ya kukosa damu huku kuna uwezekano mkubwa wa watu kujitolea kutoa damu.

Naye Mkuu wa Kitengo cha Damu Salama, Dk. Leah Kitundya alipoulizwa juu ya ukosefu wa damu amesema tatizo hilo lipo na ni kutokana na ukosefu wa bajeti kwa ajili ya kutafuta damu salama.

Amesema, kwa sasa wanashindwa kuzunguka mashuleni kutafuta damu kutokana na kutokuwepo kwa fedha ya kutosha.

“Nikweli kama walivyosema wanafunzi na baadhi ya waganga wa hospitali za wilaya damu hakuna japo tunafanya jitihada kubwa kwa ajili ya kupata damu.

“Changamoto nyingine ni wananchi kutokuwa na elimu ya kutosha juu ya utoaji damu kwa imani kuwa wakitoa damu wanaweza kupoteza maisha wakati wa utoaji wa damu,” amesema Dk. Leah.

error: Content is protected !!