WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso ameagiza kuwekwa kwa tenki kubwa la maji katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ili kuhakikisha huduma ya maji inakuwa ya uhakika wakati wote. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar…(endelea).
Aweso ametoa agizo hilo mbele ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mhandisi Antony Sanga, leo Jumatatu tarehe 7 Novemba, 2022, walipotembelea hospitali hiyo kwa lengo la kuhakikisha huduma za maji zinaendelea kuwepo na kuweka mipango mizuri kwaajili ya baadae.
Aidha Waziri huyo ameagiza DAWASA ihakikishe inapeleka maji ya uhakika kwa sasa na kusaidia uwekaji wa maji ya akiba kama tahadhari kwa baadae.
Vilevile Aweso ameilekeza Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu kutafiti haraka na kuchimba kisima ili kuwa na uhakika wa upatikanaji Maji.
Naye, Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Mohammad Janab amefafanua kuwa Hospitali inahitaji angalau akiba ya lita milioni sita.
Akitoa taarifa ya upatikanaji wa maji hospitalini hapo Katibu Mkuu Wizara ya Afya Prof. Abel Makubi ameeleza umuhimu wa kuwa na akiba ya maji ndani ya Hospitali zote nchini ili kuepusha usumbufu wowote kwa huduma za tiba kwa Wananchi.
Leave a comment