July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Uhaba BVR walalamikiwa Ipagala

Msimamizi wa mashine za kuandikisha daftari la kudumu la wapiga kura (BVR) akimuandikisha mpiga kura

Msimamizi wa mashine za kuandikisha daftari la kudumu la wapiga kura (BVR) akimuandikisha mpiga kura

Spread the love

WANANCHI wa Kitongoji cha Swaswa Bwawani katika Kata ya Ipagala, wamelalamikia uhaba wa mashine za uandikishaji (BVR) na kudai kuwa, wananchi wengi wa kitongoji hicho wasiweze kuandikishwa. Anaandika Dany Tibason kutoka Dodoma … (endelea).

Wananchi hao walitoa kauli hiyo jana walipozungumza na mwandishi baada ya kufika katika kituo kilichopo Swaswa Bwawani na kukuta watu wengi wakidai kutoandikishwa tangu zoezi hilo lianze.

Emanuel Mpuya, mkazi wa eneo hilo amesema, kuna wasiwasi mkubwa wa wananchi kutojiandikisha kutokana na uhaba wa mashine huku wananchi wa kitongoji hicho wakiwa ni wengi.

Mpuya amesema, mbali na kuwa wananchi ni wengi bado kuna utaratibu ambao wakati mwingine unawachanganya na kuwafanya wananchi kukata tamaa ya kujiandikisha.

“Mimi nimefika hapa tangu zoezi limeanza na leo (jana) ni siku ya tatu lakini sijaandikishwa, mara tunaambiwa tuandike majina wakati mwingine anasema kuwa tupange foleni. Jambo hilo linatufaya tukate tamaa kwa maana hakuna kanuni maalum.

“Mbali na hilo mashine wakati mwingine inazidiwa na tunaambiwa ni mbovu, inabidi fundi atoke mjini hadi hapa sisi wabangaizaji unadhani tunaweza kusubiri wakati tunatakiwa kukimbizana na maisha?

“Kama kweli tume ina nia ya dhati ili Watanzania wote wajiandikishe, ni bora iongeze mashine au iongeze siku za kujiandikisha vinginevyo tutakosa haki zetu.” Amesema.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Swaswa, Steven Magilanga amesema kuwa, ni kweli wananchi wa Swaswa Bwawani ni wengi na mashine za kujiandikishia ni chache wakati wananchi ni wengi.

Hata hivyo amesema kuwa, kuna baadhi ya mabalozi ambao wanaoneka kuingiza siasa katika zoezi zima jambo ambalo linakwamisha uandikishaji.

“Kuna haja kubwa ya tume kuongeza mashine ya uandikishaji BVR vinginevyo kuna uwezekano mkubwa wananchi wengi wakakosa nafasi ya kujiandikisha .

“Jambo hili ni muhimu sana kwa maisha ya Watanzania lakini serikali inalichukulia kama jambo dogo wakati lina umuhimu mkubwa zaidi.” Anasema Magilanga.

Mmoja wa msimamizi ambaye hakutaka jina lake litajwe amesema kuwa, wapo baadhi ya watu ambao wanajiita mabalozi ambao wanakuwa na majina yao na kutaka wawe wa kwanza kuandikishwa na kuwa, wamekuwa wakipingana nalo kwa kuwa wanahitaji watu wafike wenyewe vituoni.

error: Content is protected !!