Tuesday , 3 October 2023
Home Kitengo Maisha Afya Ugonjwa wa Lupasi wapigwa vita nchini
Afya

Ugonjwa wa Lupasi wapigwa vita nchini

Ummy Mwalimu, Waziri wa Afya
Spread the love

WAKATI Ugonjwa wa Lupasi unakadiria kuathiri watoto 15 kati ya watoto 52 waliopimwa serikali imeweka mikakati ya kukabiliana na ugonjwa huo ikiwa pamoja na kujenga kituo maalum. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Lupasi duniani, leo tarehe 14 Mei 2022, Mwakilishi wa Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ambaye ni Mkurugenzi wa Tiba wizarani, Dk. Pius Gerald amesema kuwa watatengeneza mpango wa kutangaza ugonjwa huo ili watu waufahamu kwa lengo la kuondoa dhana potofu ikiwemo kurogwa na unyanyapaa pamoja na kuwapatia mafunzo madaktari namna ya kuutambua ugonjwa huo.

Amesema kuwa atapeleka mapendekezo serikali ya namna ya kuwa na kituo cha pamoja cha kutibu lupasi sambamba na kuongeza wataalamu kwa lengo la kurahisisha upatikanaji wa matibabu na vipimo vya ugonjwa huo.

Kwa upande wake, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda alisema kuwa wametenga Sh bilioni moja kwa ajili ya tafiti kwenye sayansi na tiba ili kutatua matatizo kwenye jamii.

“Tunaahidi wahadhiri watakaofanya tafiti na kuzichapisha kwenye majarida ya kimataifa watapatia Sh milioni 50 kila mmoja na tutawapatia ufadhili wa masomo ya nje kwa madaktari wetu. Lakini wanafunzi watakaofanya vizuri katika masomo ya sayansi hususani PCB na PCM tutawapatia ufadhili wa asilimia 100 kusoma bure haijalishi wazazi wao wanafedha au la lengo ni kuokoa maisha ya watu,” alisema Profesa Mkenda.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adlof Mkenda

Wakati huo huo Chama cha watu wenye Ugonjwa huo nchini kimeiomba serikali kuona namna ya kupunguza gharama za dawa na matibabu sambamba na kuweka kituo kimoja cha kutibu ugonjwa huo ili kurahisisha upatikanaji wa huduma.

Inakadiriwa kuwa kati ya watoto 52 waliopimwa ugonjwa wa lupasi, wanane ambao ni wakike sawa na asilimia 15 walikutwa na ugonjwa huo na kwamba kutokana na kutogundulika mapema na kuchelewa huduma za matibabu walifariki.

Mwakilishi wa wagonjwa hao, Siwazuri Mwinyi alisema huduma za matibabu pamoja na dawa hazijajumuishwa kwenye bima za afya hivyo kuwa mzigo kwa watanzania.

‘’Bei ya chini ya kidonge cha dawa za lupasi ni ghali mnoo kuna dozi inafika mpaka shilingi Milioni sita tunaiomba serikali itupunguzie gharama hizo’’ amesema Mwinyi.

Amesema kuwa zipo changamoto nyingi zinazowakabili wagonjwa wa lupasi ikiwemo kuchelewa kupata matibabu kutokana na kukosekana kwa wataalamu wenye ubobezi kwenye ugonjwa huo.

“Mpaka mtu anagundulika na ugonjwa wa lupasi anakuwa amezungukia katika hospitali nyingi na wengine huhusisha ugonjwa huu na imani za kishirikina sababu kubwa hakuna wataalamu. Kuna wagonjwa wa lupasi ambao walianza kutibiwa na kumeza vidonge vya Kifua Kikuu na wengine ngozi lakini kumbe ugonjwa wake ni lupasi,” ameongeza Mwinyi.

Makamu Mkuu wa Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi (Muhas), Profesa Andrew Pembe amesema kuwa lengo la maadhimisho hayo ni kuongeza uelewa katika jamii na watoa huduma za afya nchini.

Alisema kuwa bado kuna changamoto ya watalaamu wa afya wanaohudumia wagonjwa wa lupasi , kwani takwimu zinaonesha kuwa kati ya wagonjwa 100,000, 70 hadi 100 wanaugonjwa wa lupasi nchini.

Amesema kuwa ugonjwa huo unasababishwa na hitilafu kwenye mfumo wa kinga ya mwili hivyo kushambulia kinga na kuathiri maeneo mbalimbal ya mwili ikiwemo figo, damu, mapafu, mgongo na ngozi.

‘’Changamoto kubwa ni vipimo vya ugonjwa huu kwani hupatikana kwa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Agakhan, TMJ, Hospitali ya Rufaa ya Bugando na KCMC. Wataalamu wengi wa afya huusisha ugonjwa huu na Ukimwi na TB hivyo, wataalamu wanaohudumia wagonjwa hawa ni wale madaktari bingwa na bobezi kwenye magonjwa ya figo, damu na mapafu,’’ alifafanua Profesa Pembe.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari Mchanganyiko

Chanjo mpya ya malaria Sh 5,000-10,000

Spread the loveShirika la afya la Duniani (WHO) limeridhia chanjo ya pili...

AfyaHabari Mchanganyiko

Wagonjwa kiharusi waongezeka, Hospitali Mkapa yaja matibabu mapya

Spread the loveHOSPITALI ya Benjamini Mkapa kwa kushirikiana na madaktari Bingwa kutoka...

AfyaHabari Mchanganyiko

Wananchi Geita wachangamkia uchunguzi wa saratani bure, wanawake wapewa neno

Spread the loveMAONESHO ya Sita ya Teknolojia ya Madini Geita yameendelea kuwanufaisha...

Afya

Serikali yaanza kutekeleza maombi ya Prof. Muhongo

Spread the loveSERIKALI imeanza kutekeleza maombi ya Mbunge wa Musoma Vijijini, Prof....

error: Content is protected !!