Friday , 29 March 2024
Home Kitengo Maisha Afya Ugonjwa wa ajabu waua watatu Lindi, wawili wapona
AfyaTangulizi

Ugonjwa wa ajabu waua watatu Lindi, wawili wapona

Mganga Mkuu wa Serikali, Dk. Alfello Sichalwe
Spread the love

 

WIZARA ya afya kupitia Mganga Mkuu wa serikali, Dk. Alfello Sichalwe imesema jumla ya watu watatu wamefariki dunia kutokana na ugonjwa wa ajabu ulioibuka mikoa ya kusini na kuthibitishwa jana na Rais Samia Suluhu Hassan.

Watatu hao ni kati ya wagonjwa 13 walioripotiwa katika kituo cha afya Mbelekenyera kilichopo kitongoji cha Naungo, kata ya Nanjilinji wilayani Kilwa mkoani Lindi. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Ugonjwa huo ambao unasababisha watu kutokwa damu puani na kuanguka, ulithibitishwa na Rais Samia Suluhu Hassan jana tarehe 12 Julai, 2022 wakati akihutubia mkutano wa Shirikisho la maaskofu wakatoliki Afrika Mashariki na Kati (AMECEA).

Alisema waziri mkuu Kassim Majawali alimweleza kuwa kuna ugonjwa huo umeibuka katika mikoa ya kusini ambako alifanya ziara.

Aidha, katika taarifa iliyotolewa leo tarehe 13 Julai, 2022 na Mganga Mkuu wa serikali imesema tarehe 7 Julai, mwaka huu wizara ya afya ilipokea taarifa kutoka kwa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Lindi kuwa katika Halmashauri ya Ruangwa kumekuwapo na ugonjwa usio wa kawaida.

Dk. Sichwale amesema ugonjwa huo uliripotiwa katika Kituo cha Afya Mbekenyea ambapo ndani ya siku tatu kuanzia tarehe 5 hadi 7 Julai, 2022 walipokea wagonjwa wawili katika kituo hicho wakiwa na dalili za homa, kuvuja damu hususani puani, kichwa kuuma na mwili kuchoka sana.

“Wizara iliunda timu ya watalaam kutoka idara ya magonjwa ya dharura na majanga, epidemiolojia, Mkemia Mkuu wa Serikali, Taasisi ya Utafiti (NIMR) waliungana na timu ya mkoa ikihusisha pia idara ya mifugo. Hadi kufikia tarehe 12 Julai, mwaka huu jumla ya wagonjwa 13, kati yao watatu wamefariki.

Amesema wagonjwa wawili waliokuwa wametengwa katika kituo cha afya Mbelekenyera wamepona na kuruhusiwa kurudi nyumbani wakati wagonjwa watano wamejitenga katika makazi yao ya muda kwenye kitongoji cha Naungo, kata ya Nanjilinji wilayani Kilwa mkoani Lindi.

Ameongeza kuwa mgonjwa mmoja ambaye amepona, anaendelea kufanya shughuli zake kijijini Mbekenyera.

Amesema watu waliotangamana na wagonjwa hao, wamekuwa wakifuatiliwa afya zao kila siku na hadi siku  saba hakuna aliyeonesha dalili zozote zinazofanana na za wagoinjwa hao lakini pia timu yawatalaam hao inaendelea na ufuatiliaji.

Pia amesema sampuli za awali zilizopimwa katika maabara ya Taifa zimeonesha majibu hasi, kwa ugonjwa wa Ebola, Marburg na UVIKO-19.

“Tunaendelea kufanya uchunguzi zaidi wa kiepidemiolojia na kitabibu, pia tunasubiri matokeo ya vipimo zaidi vya maabara ya magonwa ya binadamu, wanyama na mkemia mkuu wa serikali. Tunaendelea kutafuta watu wengine wenye dalili kama hizo ili kutambua mapema na kuwatenga ili kuzuia ugonjwa usisambae.

“Tunaendelea kuwatambua watu wote waliotangamana na wagonjwa, wahisiwa, marehemu na kuwafuatilia kwa siku 21. Kutoa matibabu kwa wagonjwa waliobainika kuwa na dalili pia kuwashauri wajitenge wakati wakisubiria majibu ya vipimo vya maabara.

“Kutoa elimu kwa jamii kwa kutumia vyombo mbalimbali vya habari na kufanya maandalizi ya dawa, vifaa tiba na vifaa vya kujikinga na maambukizi kwa ajili ya kuwahudumia waathirika endapo watajitokeza tena,” amesema.

Aidha, amesema taarifa ikikamilika, wizara itatota taarifa kamili kwa umma hivyo wananchi wawe watulivu wakati ikiendelea kulifanyia kazi suala hilo.

Amesema wananchi waendelee kutumia vituo vya kutolea huduma za afya pale wanapojisikia kuumwa.

Related Articles

KimataifaTangulizi

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the love  TUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!