Friday , 1 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Ugonjwa wa ajabu watesa wanafunzi Tanga
Habari MchanganyikoTangulizi

Ugonjwa wa ajabu watesa wanafunzi Tanga

Spread the love

WANAFUNZI wanaosoma shule ya sekondari ya Kwamkabara kata ya Kwamkabara wilayani Muheza mkoani Tanga wamepatwa na ugonjwa wa ajabu unaosababisha kuanguka hovyo, anaandika Mwandishi Wetu.

Ugonjwa huo umesababisha wanafunzi 52 mpaka 70  wanaanguka baada ya kushikwa na ugonjwa waajabu wa kuanguka na kupiga kelele pamoja na kutokwa ute mdomoni kama wamepandisha mashetani.

Tukio hilo limetokea juzi katika shule hiyo ya sekondari ya kata ya Kwamkabara wilayani Muheza mkoani Tanga. Mkuu wa shule hiyo Getrude Moyo amethibitisha kuwapo tukio hilo la watoto kuanguka na kupiga kelele.

Akizungumza eneo la tukio Ofisa elimu wa shule za msingi wilayani Muheza, Julitha Akko amesema kuwa wanafunzi hao walishikwa na ugonjwa wa kuanguka na kupiga kelele kama wamepandisha mashetani.

Akko alisema kuwa mpaka sasa chanzo cha wanafunzi hao kuanguka na kupiga kelele bado hakijafahamika na wazazi kwa kushirikiana na walimu wa shule hiyo walifanya maombi ya kukemea mapepo  katika shule hiyo na baadae wanafunzi hao kuchukuliwa na kurudi nyumbani.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Mwili wa Hayati Mwinyi kuagwa leo saa 8 Uwanja wa Uhuru

Spread the loveMWILI wa Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi unatarajiwa kuagwa kuanza...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Mwinyi kuzikwa Machi 2 visiwani Unguja

Spread the loveMWILI wa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Pili wa Tanzania,...

Habari za SiasaTangulizi

Rais mstaafu Mwinyi afariki dunia

Spread the loveRais Mstaafu wa awamu ya pili wa Tanzania, Ally Hassan...

Habari Mchanganyiko

Karafuu, Parachichi yawa fursa Morogoro

Spread the loveIMEELEZWA kuwa zao la karafuu ambalo kwa sasa linalimwa pia...

error: Content is protected !!