Saturday , 3 June 2023
Home Kitengo Maisha Afya Ugonjwa wa ajabu ulioua watano Bukoka ni Marburg
AfyaHabari

Ugonjwa wa ajabu ulioua watano Bukoka ni Marburg

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu
Spread the love

WAZIRI wa Afya, Ummy Mwalimu amesema ugonjwa wa ajabu uliosababisha vifo vya watu watano kati ya wanane waliougua wilayani Bukoba Vijijini mkoani Kagera umetambuliwa kuwa ni Marburg. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari leo jioni tarehe 21 Machi 2023, Waziri Ummy amesema ugonjwa huo hauna tiba mahususi bali hutibiwa kwa dalili husika anazokuwa nazo mtu.

Amesema ugonjwa huo huambukizwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine au kutoka kwa mnyama kwenda kwa binadamu.

Kirusi aina ya Marburg

Ameongeza kuwa hadi kufikia leo siku tano tangu kuripotiwa kwa ugonjwa huo, ni watu nane ndio wameambukizwa na vifo ni vitano vikiripotiwa huku watatu wakiendelea na matibabu,

“Tumefanikiwa kudhibiti ugonjwa huu haujatoka nje ya eneo lililolumbwa na ugonjwa huu,” amesema.

Kauli ya Waziri huyo mwenye dhamana imekuja siku chache ambapo tarehe 16 Machi 2023 na Mganga Mkuu wa Serikali, Profesa Tumaini Nagu alitangaza kuripotiwa kwa ugonjwa usiojulika katika vijiji vya Bulinda na Butayaibega vilivyopo katika kata za Marua Kanyangereko wilayani Bukoba

Hata hivyo, leo Profesa Nagu amefafanua watu hao walipata dalili za homa, kutapika, kutokwa na damu maeneo mbalimbali ya mwili na figo kushindwa kufanya kazi.

Aidha, amesema ili kudhibiti ugonjwa huo usisambae, amewataka watu kuepuka kumgusa mgonjwa au majimaji ya mwili mfano mate, machozi, damu, mkojo na kinyesi yatokayo kwa mgonjwa ama mtu mwenye dalili hizo.

“Iwapo mtu atalazimika kumhudumia mgonjwa kwa dharura, achukue tahadhari ya kujikinga majimaji yoyote kabla ya kumhudumia,” amesema.

1 Comment

  • @THINK/Dedication/Remember”@ EMPLOY THEM ALL – ALL TANZANIAN HAS JOB TO DO

    In 2021, the unemployment rate in Tanzania remained nearly unchanged at around 2.74 percent. With a decline of 0.04 percentage points, there is no significant change to 2020. Over the observed period, the unemployment rate has been subject to fluctuation.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Afya

TEMDO yaanza kuzalisha vifaa tiba, bilioni tatu kutumika

Spread the loveKATIKA kukabiliana na changamoto ya upatikanaji wa vifaa tiba nchini,...

Afya

Ummy Mwalimu:Umeme wa uhakika tija kwa uboreshaji huduma za afya

Spread the loveWAZIRI wa Afya, Ummy Mwalimu amepongeza juhudi zinazoendelea kufanywa na...

Afya

Madaktari bingwa 10 waliokuwa India warudi na shuhuda nzito kuhusu utalii tiba

Spread the loveMADAKTARI bingwa wa upasuaji wa ubongo wameendelea kuongezeka katika Taasisi...

HabariHabari Mchanganyiko

Sekta ya Mawasiliano imekuwa na maendeleo makubwa ya kiuchumi nchini-Mohamed

Spread the loveWaziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Serikali Mapinduzi Zanzibar Khalid...

error: Content is protected !!