July 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ughaibuni waguswa mauaji albino

Mwakilishi wa Diaspora, Honeymoon Aljabir (katikati) akizungumza na waaandishi wa habari.

Spread the love

WATANZANIA  waishio Marekani wameguswa na mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino), yanayotokea nchini Tanzania na kuamua kujitoa katika kupinga mauaji ya hayo. Anaandika Faki Sosi, DSJ … (endelea).

Hayo yameelezwa na Mwakilishi wa Diaspora hao Honeymoon Aljabri wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam

Amesema kuwa kukithiri kwa mauji ya albino kumewafanya washindwe kuvumilia na kuuamua kuja nyumbani Tanzania ili kuhamasisha kupinga kupitia vyombo vya habari na mitandao mbalimbali ya kijamii kwa kutoa elimu kwa jamii ya kuwalinda na kutoa ushikiano na vyombo mbalimbali vya usalama

Aljabri amesema kuwa wataanza kufanya uhamasishaji huu kwenye mkoa wa Geita kutokana na kuwa kanda hiyo imekuwa miongoni mwa sehemu zilizokithiri mauaji hayo

“ kaulimbiu ya kampeni hiyo ‘je ningekuwa mimi albino ungenihukumu kifo’ (It could be me albino) na sisi tuanajisikia vibaya sana tukiwa ughaibuni tunapoambiwa kinachoendelea nchi kwetu,” amesema.

Ameongeza kwa kuzitaka taasisi nyingine kuwaunga mkono katika kampeni hiyo

error: Content is protected !!