Friday , 19 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Uganda wakanusha kuikabidhi China uwanja wa Entebe
Kimataifa

Uganda wakanusha kuikabidhi China uwanja wa Entebe

Spread the love

 

Serikali ya Uganda na ubalozi wa China mjini Kampala wamekanusha ripoti kwamba China inaweza kuchukua udhibiti wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Entebbe. Anaripoti Rhoda Kanuti … (endelea).

Taarifa zinazokuja siku chache baada ya Gazeti la Daily Monitor la nchini Uganda kufichua masharti ya mkopo wa dola milioni 200 ( Sh bilioni 460.5) uliotolewa mwaka 2015 na benki ya China ya Exim Bank kwa ajili ya upanuzi wa uwanja wa ndege.

Aidha, Mamlaka ya usafiri wa anga ya Uganda imesema Serikali haijawahi kukabidhi uwanja wa ndege wa Entebbe kwa China.

Msemaji wa Mamlaka hiyo, Vianney Luggya mamlaka ya Uganda, siku zote, imetimiza ahadi zake kuhusu ulipaji wa mkopo uliotolewa na Benki ya China ya Exim Bank.

Lakini Joel Ssenyonyi, mkuu wa kamati ya bunge kwa mashirika ya serikali, anasema ana wasiwasi kuhusu athari ya kutolipa deni wakati kipindi cha msamaha cha miaka saba, ambapo viwango vya riba vya asilimia mbili pekee vinapaswa kulipwa, kitamalizika mwaka ujao.

Mbunge huyo pia amekosoa baadhi ya Ibara ya mkataba wa mkopo, zilizoonyeshwa bungeni na kufichuliwa kwenye vyombo vya habari, ambavyo anaona vinahatarisha uhuru wa nchi juu ya uwanja wake wa ndege pekee wa kimataifa.

Miongoni mwa njia zenye matatizo zaidi, amesema, ni uwezo wa mkopeshaji kudhibiti fedha za mamlaka ya usafiri wa anga ya Uganda. Udhibiti ambao haujawahi kuwekwa kulingana na Vianney Luggya.

Mbele ya kamati hiyo ya Bunge, Waziri wa Fedha, Matia Kasaija alikiri mwezi uliopita kuwa kuna hitilafu katika mkataba uliotiwa saini mwaka wa 2015. Lakini aliahidi serikali kuingilia kati ikiwa mapato ya uwanja wa ndege hayatoshi kulipa mkopo huo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Tetemeko la ardhi laua 7, lajeruhi 800 Taiwan

Spread the loveWatu wapatao saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 800...

error: Content is protected !!