February 25, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Uganda kwazidi kuchafuka

Spread the love

MTU mmoja amepoteza maisha na zaidi ya watu 100 wamekamatwa na Jeshi la Polisi nchini Uganda, katika maandamano yaliyozuka kwa ajili ya kupinga kukamatwa kwa mbunge wa upinzani, Robert Kyagulanyi ‘Bob Wine’. Anaripoti Regina Kelvin … (endelea).

Polisi nchini Uganda jana tarehe 20 Agosti, 2018 ilitumia nguvu kuzuia maandamano hayo yaliyofanyika mji mkuu wa Uganda, Kampala.

Katika fujo hizo, waandamanaji hao walichoma moto matairi, waliweka vizuizi barabarani pamoja na kurusha mawe.

Bobi Wine alikamatwa na kushtakiwa kwenye mahakama ya kijeshi wiki iliyopita kufuatia madai kuwa alikuwa anamiliki silaha kinyume cha sheria.

error: Content is protected !!