Wednesday , 24 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Ufugaji wa Sungura na kukua kwa mnyonyoro wa thamani wa mkulima
Habari Mchanganyiko

Ufugaji wa Sungura na kukua kwa mnyonyoro wa thamani wa mkulima

Hyasinta Minde
Spread the love

UFUGAJI wa mnyama Sungura umekuwa na faida nyingi bila watu kujua duniani na hivyo kubaki wakifuga wanyama wengine. Anaripoti Christina Haule, Morogoro … (endelea).

Hyasinta Minde ni Afisa Mifugo kutoka SUA ambaye anaeleza faida za ufugaji wa Sungura kama wanyama wanaoweza  kusogeza mbele mnyororo wa thamani na kuongeza kipato kwa wafugaji ambapo anasema licha ya mauzo ya mnyama huyo kuwa ni ya bei juu lakini pia mfugaji anaweza kunufaika kwa kuuza mkojo kama dawa ya kuua wadudu kwenye mbogamboga na matunda.

Minde anasema licha ya faida ya nyingine ya kufuga Sungura kuwa ni nyama lakini mfugaji anaweza kufuga Sungura wengi apendavyo na kuweka vifaa vya kutegea mkojo ambao atauhifadhi kwa usafi na baadae kupaki kwenye chupa na kuweza kuuza kwa wakulima au kufanya matumizi ya kilimo yeye mweneywe.

Anasema, lita moja ya mkojo wa Sungura huuzwa kwa shilingi 10,000 za kitanzania ambapo akiwa na Sungura wapatao 20-30 anaweza akakusanya mkojo ndani ya miezi 6 anaweza kupata lita 12 na kuuza kwa wakulima  na kujipatia sh 120,000 na kukuza uchumi wake na Taifa kwa ujumla huku akifikia uchumi wa kati unaokusudiwa kwa sasa.

Aidha Minde anasema pia kinyesi cha Mnyama Sungura kinaweza kuwa biashara nzuri kwa mfugaji pia kufuatia kuuzwa kwa  shilingi 250 za kitanzania kwa kilo 10 za kinyesi cha Sungura.

Minde anasema, Sungura mmoja anaweza kuuzwa kwa kiasi cha shilingi inategemea na mahali anapouzwa au alipofugwa sambamba na ubora wake.

Anasema, zipo aina nyingi za Sungura ikiwemo California white, German Giants, Newsland White, American Sports, Angola, kutch na chinchilla ambao wanapatikana SUA kwa sasa.

Afisa huyo anasema Sungura mmoja anabeba mimba kwa siku 8-35 wastani wa mwezi mmoja na anaweza kuzaa watoto wasiopungua 8-12 kwa uzao mmoja ambapo kwa ufugaji uliobora anaweza kuzaa mara 5 kwa mwaka na hivyo mfugaji kuwa na wastani wa Sungura 40 .

Anasema ipo faida kubwa katika ufugaji wa wanayama hao kutokana na kwamba hawampi mfugaji mawazo kufuatia kula pumba tu na maji na kuendelea kukua.

Minde anasema ufugaji wa Sungura hadi kukua unachukua miezi 8-12 na kuwa tayari kwa kuliwa iwe kwa Sungura wa kizungu (Broiler) au wa kienyeji.

Anasema nyama ya mnyama huyo inafanana na nyama ya Kuku ambayo ni sehemu ya nyama nyeupe inayofaa kuliwa na kila mtu na kumuongezea protini mwilini.

Aidha Minde anasema Sungura anatakiwa kuepushwa na majimaji wakati anapofugwa ambapo mabanda yao yanapaswa kuwa juu juu na kuwa na sehemu ya chini ya kushusha mkojo na kinyesi.

Minde anasema zipo changamoto zinazompata mnyama Sungura wakati wa ufugwaji ambao zi pamoja na magonjwa ya kuhara damu na minyoo ya ngozi ambayo kwa ujumla yanatibika kwa kutumia dawa kutoka kwa maduka ya dawa za mifugo.

Hata hivyo anasema mkojo wa Sungura kama dawa ya kuua vijidudu waharibifu wa mbogamboga na matunda hauleti madhala kama mtumiaji atatumia kwa kufuata ushauri anaopewa.

Hivyo aliwataka wakulima na wafugaji kutembelea banda la maonesho ya wakulima la Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) lililopo kwenye sherehe za wakulima 88 Kanda ya Mashariki kupata elimu juu ya ufugaji wa Sungura kwa faida na elimu zingine.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

THRDC yaongeza mkataba wa ushirikiano na ABA

Spread the love  MTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC),...

Habari Mchanganyiko

Rufaa ya Equity Benki, State Oil yakwama

Spread the loveMAHAKAMA ya Rufani, jijini Dar es Salaam, imeshindwa kuendelea na...

Habari Mchanganyiko

Bodaboda waeleza mafanikio mafunzo usalama barabarani

Spread the loveMADEREVA bodaboda katika Jiji la Dodoma wameeleza jinsi mafunzo ya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yaahidi kuendelea kuunga mkono Serikali za Mitaa

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imesisitiza dhamira yake ya...

error: Content is protected !!