December 3, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ufaulu darasa la saba wapaa kwa miaka minne mfululizo

Spread the love

UFAULU wa mtihani wa darasa la saba nchini umeongezeka maradufu kwa miaka minne mfululizo kuanzia mwaka 2015 ambapo ufaulu ulikuwa asilimia 56.99 hadi 77.72% kwa mwaka 2018. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa na Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA), kwa mwaka 2018, ufaulu umeongezeka kwa asilimia 4.96 kutoka asilimia 72.76 ilivyokuwa mwaka 2017 hadi 77.72% mwaka huu.

Katika kipindi cha mwaka 2018, takwimu zinaonyesha ufaulu katika masomo ya Maarifa ya Jamii, Kiingereza, Sayansi na Hisabati umepanda kwa asilimia kati ya 4.03 na 11.92 wakati somo la Kiswahili ufaulu wake ukishuka kwa asilimia 1.44 ikilinganishwa na ufaulu ulivyokuwa mwaka 2017.

Ufaulu wa mwaka 2017 nao pia uliongezeka kwa asilimia 2.40 kutoka asilimia 70.36 ilivyokuwa mwaka 2016 hadi kufikia 72.76% ilivyokuwa mwaka 2017.

Katika kipindi cha mwaka 2017, ufaulu katika masomo ya Kiswahili, Kiingereza na Hisabati ulipanda kwa asilimia kati ya 4.25 na 10.05 ukilinganisha na ufaulu wa mwaka 2016.

Vile vile, ufaulu wa mwaka 2016 ulipanda kwa asilimia 2.52 kutoka asilimia 67.84 ilivyokuwa mwaka 2015 hadi kufikia asilimia 70.36 kwa mwaka 2016.

Hali kadhalika, ufaulu wa mwaka 2015 ulipanda kwa asilimia 10.85 kutoka asilimia 56.99 ilivyokuwa mwaka 2014 hadi kufikia asilimia 67.84 kwa mwaka 2016.

Screen Shot 2018-10-23 at 3.31.19 PM

error: Content is protected !!