November 29, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Ufaulu darasa la saba waongezeka kwa 6.69% , Kiswahili chang’ara

Dk. Charles Msonde, Katibu Mtendani wa NECTA

Spread the love

 

BARAZA la Mitihani Tanzania (NECTA), limesema asilimia 81.97 ya wanafunzi 1,107,460, waliotunukiwa matokeo ya mtihani wa darasa la saba, uliofanyika tarehe 8 na 9 Septemba 2021, wamefaulu mtihani huo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Matokeo hayo yametangazwa leo Jumamosi, tarehe 30 Oktoba 2021 na Katibu Mtendaji wa NECTA, Dk. Charles Msonde.

Dk. Msonde amesema, watahiniwa 907,820 kati ya 1,107,460, wamefaulu mtihani huo wa kumaliza elimu ya msingi, ambapo wamepata kati ya alama 121 hadi 300.

“Idadi hii ya watahiniwa waliofaulu ni sawa na asilimia 81.97, ya waliofanya mtihani. Ukiangalia hawa waliofaulu, wasichana wako 467,967 ambao ni sawa na asilimia 81.43 na wavulana waliofaulu wako 439,835, sawa na asilimia 82.56,” amesema Dk. Msonde.

Katibu Mtendaji huyo wa NECTA amesema, ufaulu wa mtihani huo umeongezeka kwa watahiniwa 74,130, kutoka 833,672 ilivyokuwa 2020 hadi 907,820 wa mwaka huu, ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 6.69.

Dk. Msonde amesema, twkimu za ufaulu wa kimasomo zinaonesha kuwa, ufaulu wa masomo yote uko juu ya wastani isipokuwa wa somo la Kingereza, ambao uko chini ya wastani wa asilimia 48.02.

Huku ufaulu wa somo la Kiswahili ukifanya vizuri, ambapo ulikuwa ni asilimia 88.50.

error: Content is protected !!