July 3, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ufaransa yaeleza inavyotumia njia jumuishi uhifadhi

Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Nabil Hajlaoui

Spread the love

 

BALOZI wa Ufaransa nchini Tanzania, Nabil Hajlaoui, amesema kwa miaka 60 ya uhifadhi katika nchi hiyo wamekuwa wakitumia njia ya kushirikisha wananchi wa maeneo husika. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Balozi huyo ameeleza hayo leo Jumatano tarehe 22 Juni, 2022 wakati akichangia mjadala katika mkutano wa mtandaoni, kuhusu uwekaji wa alama za mipaka tarafa ya Loliondo na maendeleo ya zoezi la uhamaji wa hiari kwa wakati wa Ngorongoro.

Mratibu wa mkutano huo alimtaka balozi Hajlaoui kuelezea uzoefu wa Ufaransa juu ya nia nzuri ya kutunza maeneo ya hifadhi na mazingira kwa ujumla na namna ya kuvutia watalii zaidi.

Balozi Hajlaoui amesema Ufaransa ina hifadhi 170 na zote zimekuwa zikiendelezwa kwa njia Jumuishi ya wananchi wa maeneo zilipo kwa lengo la kuinua uchumi wa maeneo hayo.

Amesema mbali na uhifadhi wamekuwa wakibuni mbinu za kuongeza thamani ya maeneo hayo ili yaweze kuvutia uwekezaji na watalii.

“Tunachofanya ni kuongeza thamani ya vitu vya maeneo hayo ikiwemo vyakula vya asili ya maeneo husika pamoja na tamaduni zao ili ziweze kuvutia watalii na wao kujipatia kipato na kukuza uchumi wao,” amesema.

Amesema amaeneo hayo yanasimamiwa na taasisi za kijamii za maeneo husika katika kuhakikisha yanaendelea kuhifadhiwa na kuvutia zaidi ili yaweze kuwanufaisha zaidi.

Amesema mbinu hiyo imesaidia maeneo hayo kwa miaka 60 kuendelea kuhifadhiwa na kuvutia zaidi huku uchumi wake ukikua zaidi.

error: Content is protected !!