Tuesday , 27 February 2024
Home Kitengo Maisha Elimu UDSM wafunguka ‘kufeli’ kwa Rais wa DARUSO
Elimu

UDSM wafunguka ‘kufeli’ kwa Rais wa DARUSO

Profesa Allen Mushi Mkurugenzi wa Shahada za awali katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM)
Spread the love

MENEJIMENTI ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), imesema kwa sasa haiwezi kutoa ufafanuzi wowote kuhusiana na taarifa za Erasmi Leon, aliyekuwa Rais wa Serikali ya wanafunzi wa chuo hicho DARUSO kufukuzwa masomoni kwa kufeli mitihani, anaandika Faki Sosi.

Taarifa za kiongozi huyo wa wanafunzi kufeli mitihani na kuwa mbioni kuondolewa masomoni, zilisambaa tangu jana, huku mtandao huu ukidokezwa na chanzo cha kuaminika kuwa suala hilo ni la kweli, ingawa bado uamuzi wa mwisho haujatolewa.

Akizungumza katika mahojiano na MwanaHALSI Online Profesa Allen Mushi, mkurugenzi wa Shahada za awali wa UDSM amesema matokeo ya wanafunzi yaliyotolewa Septemba mwaka huu ni ya awali na kwamba Oktoba mwaka huu, ndipo kikao cha mwisho cha kupitisha matokeo kitakaa.

“Matokeo yaliyotolewa na college (ndaki) ni provisional results (matokeo ya awali), Kama yanaonesha amefeli, hayo si matokeo ya mwisho. Kikao cha (Senate) kitakachopitisha matokeo ya mwisho kitakaa Oktoba 6 mwaka huu,” amesema Prof. Mushi.

Kuhusu taarifa zinazodai kuwa, uongozi wa chuo hicho unapanga kubadili matokeo ya Erasmi Leon, Prof. Mushi amekana madai hayo na kusema kikao cha Seneti ya UDSM ni cha kawaida kwa mujibu wa utaratibu wa upitishaji wa matokeo.

Kwa upande wake Erasmi, aliyekuwa Rais wa Serikali ya wanafunzi 2016/2017 ameiambia MwanaHALISI Online kuwa, atazungumzia kiundani kuhusu suala la matokeo yake baada ya kikao cha mwisho, huku akisema si vyema umma kumhukumu kwa matokeo ya sasa kwani yanaweza kubadilika.

“Matokeo hayajawa rasmi kwasababu hayajapitishwa na kikao cha mwisho. Katikati hapo kuna marekebisho ambayo yanaweza kufanyika kwa utaratibu tu wa kawaida. Subiri mpaka tarehe 06 Oktoba, mwaka huu, baada ya hapo nitazungumza.

Alipoulizwa na mwandishi ikiwa kuna matatizo yoyote yaliyokuwa yakimkabili kiasi cha kumuathiri kimasomo na sasa kuwa kwenye hatihati ya kufukuzwa masomoni, Erasmi amesema;

“Kila kinachotokea kina sababu zake. Nisije nikazungumzia chochote halafu baadaye kikaja kuwa kinyume, Huwezi kujua kama hili lililotokea lina sababu zake, kulizungumza kwa wakati huu haiondoi ukweli wa jambo. Ni vyema tusubiri.”

Suala la Rais wa Serikali wa wanafunzi kudaiwa kufeli masomo yake na hivyo kuwa kwenye hatihati ya kufukuzwa masomo, limetawala mitandao mingi ya kijamii kwa siku mbili sasa, huku wanafunzi wengi wa UDSM wakionesha kushitushwa na jambo hilo.

“Rais wa chuo anapaswa awe mfano kwa wanafunzi anaowaongoza kuanzia nidhamu, tabia na hata kitaaluma. Taarifa za Erasmi Leon kufeli mitihani zimetushtua ila zinatukumbusha, kwamba kuwa kiongozi wa wanafunzi, haimaanishi kuacha jukumu la kusoma,” ameeleza kiongozi wa DARUSO akiomba kutotajwa jina.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Elimu

Takukuru wambana Mwalimu mkuu, atema bungo

Spread the loveMwalimu Mkuu wa shule msingi Hanihani, kata ya Igunga wilayani...

ElimuHabari za Siasa

Prof Muhongo ataka ubunifu mitaala mipya ya elimu

Spread the loveSERIKALI imetakiwa kuhakikisha  maarifa, ujuzi, uvumbuzi na udadisi vinazingatiwa kwenye...

BiasharaElimu

NMB yatoa vifaa saidizi kwa walimu, wanafunzi wenye ulemavu Ilala

Spread the loveBENKI ya NMB, imekabidhi msaada wa vifaa saidizi kwa walimu...

Elimu

St. Mary’s Mbezi Beach High School yafanya maajabu kidato cha nne

Spread the love  WANAFUNZI waliomaliza  kidato cha nne kwenye shule ya sekondari...

error: Content is protected !!