September 29, 2021

Uhuru hauna Mipaka

UDP yamtwika mzigo Ole Medeye

Spread the love

GOODLUCK Ole Medeye, mwanasiasa mpya katika Chama cha UDP, leo ametunukiwa cheo cha Kaimu Katibu Mkuu wa chama hicho, anaandika Pendo Omary.

Kamati Kuu ya UDP imetoa uamuzi huo leo baada ya kufanya kikao chake jana ikiwa ni pamoja na kujadili mambo mbalimbali ya chama hicho.

Kamati hiyo pia imteua Andrew Bomani ambaye ni mtoto wa jaji maarufu Mark Bomani kuwa Mkurugenzi wa Mikakati ya Chama na Uhusiano wa Kimaitaifa, cheo ambacho awali hakikuwepo na kuwa, kimepatikana baada ya kufanya marekebisho ya Katiba.

Ole Medee alikuwa mwanachama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambapo siku saba zilizopita alihamia UDP na kukabidhiwa kadi ya uanachama.

Mwanasiasa huyo aliwahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Arumeru Magharibi, pia aliwahi kuwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi katika Serikali ya Awamu ya Nne.

Ndani ya vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) Ole Medeye aliteuliwa kuwania nafasi ya Uspika wa Bunge.

“Nimekubali uteuzi huu kwa moyo mkunjufu. Nitatumia ubunifu wangu kutekeleza malengo ya chama,” amesema Medeye wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi Kuu ya UDP akwia na mwenyekiti wa chama hicho, John Cheyo.

Akizungumza kuhusu Jeshi la Polisi nchini kupiga marufuku mikutano ya kisiasa na maandamano Medeye amesema, hatua hiyo ni ya kudidimiza demokrasia nchini.

“Huku ni kudumaza vyama visikue. Tunashuhudia mjadara wa bajeti wa chama kimoja. Natoa wito kwa rais kwamba, taarifa za kintelejensia anazopewa azichunguze.

“Ikiwezekana aingilie suala hili. Kufanya mikutano ni haki yetu ya kikatiba ila kama kuna vyama vya siasa vinafanya funjo, vifungiwe,” amesema Ole Med eye.

Pia Ole Medeye amemtaka msajili wa vyama vya siasa nchini kuingilia kati suala hilo kwa kuwa, ukatazwaji huo unaliweka taifa njia panda.

Hata hivyo, Cheyo amewataka viongozi hao wapya kufanya kazi ikiwa ni pamoja na kutoitukana serikali.

“Kamati Kuu ya jana haijakosea kuleta majembe, msiende kwa wananchi kutukana serikali,” amesma Cheyo.

error: Content is protected !!