October 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

UDOM yaanza kutoa msaada wa kisheria bure

Spread the love

KITUO cha Msaada wa Kisheria kutoka Chuo Kikuu cha Dododoma (UDOM), kimeanza kutoa huduma ya elimu ya sheria bure kwa wakazi wa jiji hilo. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Mbali na kutoa huduma hiyo, chuo hicho kimeahidi kutoa bure mawakili katika kuwatetea watu ambao hawana uwezo wa kutafuta kuwalipwa.

Uzinduzi wa huduma hiyo umefanywa leo tarehe 29 Januari 2020, katika viwanja vya kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere jijini humo, ikiwa ni maandaliziya Wiki ya Sheria inayotarajiwa kuanza tarehe 31 Januari 2020.

Dk. Amani Tegambwage, Kaimu Rais wa Ndaki ya Taaluma za Biashara na Sheria UDOM amesema, huduma hiyo ni bure.

 ‘’Sisi kama wanasheria, tumeamua kutumia elimu na ujuzi tulionao kusaidia wenzetu kwa kutoa msaada wa kisheria, kwani kuna watu wengi wenye matatizo, hawajuhi pa kupeleka matatizo yao na wakati mwingine hawana uwezo wa kuonana na wanasheria,” amesema Dk. Tegambwage.

Dk. Ines Kajiru, Mkuu wa Idara ya Sheria Ndaki ya Taaluma za Biashara na Sheria chuo hapo amesema, katika kutoa msaada wa kisheria, wamebaini kuwa watu wengi hawana elimu juu ya haki zao za umiliki wa ardhi, ndoa na miradhi.

Na kwamba, katika maeneo mengi wanakumbana na kesi za migogoroya ardhi, masuala ya ndoa pamoja na mambo ya miradhi, na watu wengi hawana ufahamu juu ya kudai haki zao.

“Kutokanana hali hiyo, sisi tumekuwa tukitoa elimu kwa jamii ili kuweza kuwafundisha njia ambazo wanaweza kudai haki zao kwa mujibu wa sheria.

“Na makakati wetu mkubwa ni kuhakikisha tunawafikia watu wote hasa wale walioko kijijini, asilimia kubwa hawajui sheria na haki zao zinapotea bila kujua na wengine hawana uwezo wa kuwalipamawakili wanaoweza kuendesha kesi zao,” amesema Dk. Ines.

Mwisho. 

error: Content is protected !!