Friday , 2 June 2023
Home Kitengo Maisha Elimu UDOM: China iwe mfano kwetu
ElimuHabari Mchanganyiko

UDOM: China iwe mfano kwetu

Baadhi wa wanafunzi walioshinda shindalo na kuongea lugha ya kichina
Spread the love

CHUO Kikuu cha Dodoma (UDOM), kimewataka Watanzania kuwaiga Wachina katika kuthamini na kudumisha tamaduni ikiwemo lugha ya taifa lao. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Akizungumza jijini Dodoma wakati wa mashindano ya uelewa wa Kichina, kwa wanafunzi wa shule za sekondari uliohusisha maswali, hutuba pamoja na vipaji mbalimbali, Profesa Alexander Makuliko, Naibu Makamu Mkuu wa UDOM, upande wa taaluma na tafiti amesema, Watanzania wakifuata nyayo hizo, Kiswahili kitakua duniani kote.

“Kiswahili kwa sasa kinatumia Afrika Kusini na katika Bara la Afrika kuna nchi nyingi zinatumia lugha hii kama Kenya, Uganda.

“Ni lugha ya kimataifa hivyo ni lazima tuweze kuitumia kueleza utamaduni, kuweza kuipenda nchi yetu na kuonesha kuwa, tunaweza kufanya jambo fulani kwa lugha hii katika ngazi za kimataifa,” amesema Prof. Makuliko.

Akizungumzia lugha ya Kichina katika ukuaji wa uchumi nchini Prof. Makuliko amesema, nchini ya China ni taifa moja wapo kubwa ulimwenguni lenye nguvu ya kiuchumi ambalo limekuwa likiwezeka katika maeneo mbalimbali hapa nchini.

Amesema, kutokana na fursa hizo ni lazimi Watanzania kujifunza Kichina ili kunufaika katika miradi hiyo.

Mkurugenzi mkazi wa taasisi ya Confucius inayofundisha lugha ya Kichina UDOM, Dk Rafiki Sebonda amesema, yapo masuala la tekinolojia kwa lugha ya kichina hivyo kuwepo wa Watanzania wanaojifunza kichina itasaidiakata katika mikata.

“Kama lugha huijui, unaweza kuingi mikataba ambayo hujui imeandikwa nini, kwa hiyi ni wakati muafaka wa kujifunza kichina, wakati huo huo tunahakikisha lugha yetu ya Kiswahili inatumika sehemu nyinge na inakua.

Mkurugenzi wa taasisi ya Confucius Dk Yang Lun amesema, washindi wa shindano la sita nchini, watashiriki shindano ya 12 nchini China mapema mwaka huu na watapata nafasi ya kufahamiana zaidi na wanafunzi wengine kutoka mataifa mbalimbali.

Mashindano hayo yaliyoshirikisha wanafunzi 11 kutoka shule mbalimbali nchini zinazofundisha lugha hiyo, ambapo Maureen Mwasongwe kutoka Shule ya Sekondari, Shaaban Robert iliyopo Dar es Salaam na Amina Kibao kutoka Shule ya Sekondari Rosmin, Tanga walikuwa washindi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Serikali yakabidhi eneo la mahakama ya Afrika ya haki za binadamu

Spread the loveSerikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa...

Habari Mchanganyiko

Udhamini wa NMB mikutano ya ALAT wafikia 1.2 bilioni

Spread the loveBENKI ya NMB imeendelea kufanya kazi kwa karibu na Asasi...

Elimu

Serikali yatoa Sh. 573 mil. kukamilisha wa ujenzi sekondari ulioanzishwa na wanakijiji

Spread the love  SERIKALI kupitia Wizara ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI, imetenga Sh....

Habari Mchanganyiko

Dk. Gwajima atoa maelekezo kwa maofisa maendeleo nchini

Spread the love  WAZIRI wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia Watoto,...

error: Content is protected !!