Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Udhaifu vituo vya utafiti wamuinua Sugu bungeni
Habari za Siasa

Udhaifu vituo vya utafiti wamuinua Sugu bungeni

Spread the love

MBUNGE wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (Sugu) kutoka Chadema ameiomba serikali kueleza ni lini itatenga fedha za kutosha kwa ajili ya kufufua vituo vya utafiti kama vile Chuo cha Utafiti kilichopo Uyole, Mbeya. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma…(endelea).

Akiuliza swali la nyongeza bungeni Mbilinyi amesema kuwa, kwa sasa Chuo cha Uyole kinakabiliwa na miundombinu pamoja na ufinyu wa bajeti.

Amehoji, lini serikali itaweza kuweka mipango ya kuongeza bajeti ili kuweza kufanya chuo hicho kuwa na miundombinu pia kukiongezea bajeti ili kiweze kufanya vizuri zaidi.

Katika swali la msingi la Martin Msua, Mbunge wa Mbinga Vijijini (CCM) aliyetaka kujua ni lini serikali ilifanya utafiti wa gharama za uzalishaji wa kahawa wilayani Mbinga kwa mara ya mwisho.

Akijibu maswali hayo Omar Mgumba, Naibu Waziri wa Kilimo amesema, serikali ilipeleka mswada wa Sheria bungeni na kuunda vituo 16 ambapo kila kituo kitakuwa kikifanya utafiti wa mazao mawili tu.

Mgumba amesema, lengo la kufanya kila kituo kufanya utafiti wa ni kufanya vituo hivyo visiweze kulemewa katika utendaji wao wa kazi.

Akizungumzia suala la kuwezesha kituo kikubwa cha Utafiti cha Uyole amesema, katika bajeti ya mwaka wa fedha 2019/20 watakitengea fedha chuo hicho.

Mgumba amesema kuwa, serikali katika mwaka wa fedha 2015/2016 kupitia taasisi ya Utafiti wa Kahawa Tanzania (TaCRI) imefanya utafiti wa uzalishaji wa kahawa katika wilaya saba;- Mbinga, Mbozi, Tarime,Rombo, Muleba, Karagwe na Buhigwe.

Amesema, utafiti uliofanywa na TaCRI kwa wakulima wa kahawa aina ya Arabca unaonesha gharama za uzalishaji wa aina bora za kahawa zenye ukinzani wa magonjwa Sh. 2.1 Mil kwa heka sawa na wastani wa Sh. 843.4 kwa kilo zenye tija ya wastani wa kilo 2662 kwa hekta.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

Habari za Siasa

CCM yamkana mwenyekiti UVCCM aliyetaka wapinzani wapotezwe

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimejitenga na kauli ya mwenyekiti...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia kutunukiwa udaktari wa heshima Uturuki

Spread the loveBaraza la Chuo Kikuu cha Ankara, ambacho ni cha pili...

error: Content is protected !!