October 23, 2021

Uhuru hauna Mipaka

UCSAF kuunganisha shule kwa inteneti

Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia profesa Makame Mbarawa, akizungumza na waandishi wa habari. (hawapo pichani)

Spread the love

MFUKO wa mawasiliano kwa wote (UCSAF), umesaini mikataba ya miradi miwili ya upelekaji mawasiliano vijijni na maeneo maalumu ya mipakani awamu ya pili, na mradi wa kuunganisha intaneti kwenye shule za umma. Anaandika Sarafina Lidwino… (endelea)

UCSAF ni muunganiko wa kampuni nne za mawasiliano nchini za Vodacom, Tigo, Aitel, TTCL.

Akizungumza na waandishi katika hafla hiyo, Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof. Makame Mbarawa, amesema Serikali iliamua kunzisha UCSAF kwa lengo la kupeleka mawasiliano vijijni na maeneo yote yasiyo na mvuto wa kibiashara  kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa mawasiliano.

Amesema, 15 Novemba 2014, UCSAF ilitangaza zabani ya kupeleka mawasiliano ya simu katika mikoa mbalimbali ya vijijni yaliyokuwa yameainishwa na mfuko, ambapo jumla ya kata 102 kati ya 158 zilizotangazwa zilipata wazabuni wa kupeleka mawasiliano.

Wazabuni waliojitokeza kupeleka mawasiliano ni Vodacom iliyochukua kata 36, Tigo 42, TTCL 19 na Airtel 5.

Prof. Mbarawa ameongeza, “tarehe 26 Januari 2015, tulitangaza zabuni nyingine ya kupeleka mawasiliano ya simu kwenye maeneo 12 ya mipakani na maeneo maalum, jumla ya kata 10 kati ya 12 zilipata watoa huduma wa Vodacom kata 2, Tigo 5 na Aitel 3.” 

“Kuna baadhi ya makampuni hayafanyi vizuri, bado zinalegalega katika utendaji wake. Nichukue fursa hii kuwaambia kwamba wanatakiwa kuwa makini na kama hawatatekeleza makubaliano yetu tutaanza kuwashughulikia na ikiwezekana watafungiwa kabisa,” amesema Prof. Mbarawa

Amesema, Serikali inatambua umuhimu na uwepo wa UCSAF, pia inaona mchango wake katika masuala ya ajira, na hadi hivi sasa takribani Watanzania laki mbili wameajiriwa na kampuni za mawasiliano na wengine wanaokadiliwa kufika milioni tano wanategemea uwepo wa kampuni hizo.

Katika hatua nyingine, imeelezwa kuwa UCSAF ulikuwa na mazungumzo ya muda mrefu na kampuni ya mawasilano kwa njia ya Satellite ya Avanti kwa ajiri ya kuziunganisha shule za serikali na mtandao wa intaneti.

Mazungu hayo yamefikia mwisho leo, ambapo kampuni hiyo imesema shule za serikali 250 zitaunganishwa na intaneti na vituo 25 vya mafunzo ya Tehama vitaanzishwa kwa ajili ya kuwafundishia waalimu.

Mkuu wa uendeshwaji wa kampuni ya Avanti, Mathew O’Connor amesema mradi huo umegharimu takribani Sh. 8 bilioni, ukitarajiwa kumalizika mwakani.    

error: Content is protected !!