Sunday , 5 February 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa Uchunguzi Covid-19: China yaigomea WHO
Kimataifa

Uchunguzi Covid-19: China yaigomea WHO

Naibu Waziri wa Afya wa China, Zeng Yixin
Spread the love

 

SERIKALI ya China, imepinga mpango wa Shirika la Afya Duniani (WHO), wa kurudia uchunguzi dhidi ya mlipuko wa kwanza wa Virusi vya Corona. Inaripoti BBC … (endelea).

Katika mpango wake huo, WHO inataka kukagua maabara ambazo virusi hivyo viligundulika kwa mara , Desemba 2019, zilizopo kwenye Jiji la Wuhan nchini humo.

Akizungumza na wanahabari jana tarehe 23 Julai 2021, Naibu Waziri wa Afya wa China, Zeng Yixin, alisema hawatakubali uchunguzi huo, kwa madai kwamba unakiuka itifaki za maabara za nchi hiyo.

“Tunatumaini kwamba WHO itapitia kwa uzito mapitio na maoni yaliyotolewa na wataalamu wa China. Na kulichukulia janga hili kama suala la kisayansi na kuondoa uingiliaji wa kisiasa,” alisema Zeng.

Watalaamu wa WHO walitembelea Jiji la Wuhan nchini China, Januari 2021, kwa ajili ya kufanya uchunguzi katika maabara zinazoshukiwa kuzalisha virusi hivyo.

Mkuu wa WHO, Dk. Tedros Adhanom Ghebreyesus

Mkuu wa WHO, Dk. Tedros Adhanom Ghebreyesus, aliiomba Serikali ya China itoe ushirikiano katika uchunguzi huo, ambao ungehusisha taasisi za utafiti wa kisayansi.

Dk. Tedros aliitaka China iwe wazi na kushirikiana na wachunguzi wa WHO, ikiwemo kutoa data za wagonjwa ambazo hazijashirikishwa katika uchunguzi wa kwanza uliofanywa na shirika hilo.

Tangu mlipuko wa virusi hivyo utokee mwishoni mwa 2019 na kusababisha ugonjwa wa homa kali ya mapafu (Covid-19), umeuwa watu takribani milioni nne duniani.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Papa Francis kukutana na wahanga wa vita Sudan Kusini

Spread the love  KIONGOZI wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis leo Jumamosi...

Kimataifa

Polisi ahukumiwa kifo kwa kumuua wakili

Spread the love  MAHAKAMA kuu nchini Kenya imemhukumu kifo Ofisa wa Polisi,...

Kimataifa

Hospitali za China zilifurika wagonjwa, wazee kipindi cha wa likizo ya Mwaka Mpya wa Lunar

Spread the loveHOSPITALI  nchini China zimejaa wagonjwa na wazee katika kipindi cha...

Kimataifa

Papa Francis ayataka mataifa ya nje kuacha kupora mali DRC

Spread the love  KIONGOZI wa kanisa Katoliki Papa Francis, ameyataka mataifa ya...

error: Content is protected !!