Wednesday , 24 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Uchumi wa Tanzania waongezeka kwa asilimia 0.1
Habari za Siasa

Uchumi wa Tanzania waongezeka kwa asilimia 0.1

Dk. Mwigulu Nchemba, Waziri wa Fedha na Mipango
Spread the love

UCHUMI wa Tanzania umeongezeka kwa asilimia 0.1 kwa kipindi cha mwaka mmoja. Anaripoti Mwandishi Wetu Dodoma … (endelea).

Uchumi wa Tanzania umeongezeka kwa asilimia 0.1 baada ya kukua kwa asilimia 4.9 katika kipindi cha Januari hadi Septemba 2021 ikilinganishwa na ukuaji wa asilimia 4.8 katika kipindi kama hicho mwaka 2020.

Hayo yamebainishwa leo katika maelezo ya Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Nchemba, wakati akiwasilisha mapendekezo ya serikali ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2022/23 na mfumo na ukomo wa bajeti ya serikali kwa mwaka 2022/23.

“Uchumi wa Tanzania umeendelea kuimarika ambapo katika kipindi cha Januari hadi Septemba 2021 ukuaji wa uchumi wa Taifa ulikuwa asilimia 4.9 ikilinganishwa na ukuaji wa asilimia 4.8 katika kipindi kama hicho mwaka 2020,” Dk. Nchemba.

Aidha amesema ujazi wa fedha ulikua kwa wastani wa asilimia 10.2 mwaka 2021 ikilinganishwa na asilimia 8.8 mwaka 2020 huku riba ya mikopo ikipungua na kufikia wastani wa asilimia 16.59 mwaka 2021 ikilinganishwa na asilimia 16.66 mwaka 2020.

Amesema mikopo kwa sekta binafsi ilikua kwa asilimia 10 Desemba 2021 ikilinganishwa na asilimia 3.1 Desemba 2020.

Aidha akiba ya fedha za kigeni ilikuwa dola za Marekani bilioni 6.4 Desemba 2021 kiasi kinachotosheleza kuagiza bidhaa na huduma nje ya nchi kwa kipindi cha miezi 6.6 ikilinganishwa na dola za Marekani bilioni 6.0 zilizotosheleza uagizaji wa bidhaa na huduma nje ya nchi kwa kipindi cha miezi 5.6 Desemba 2020.

1 Comment

  • Grazie mwigulu sisi sote tunakupongeza kwa juhudi zako wizara ya fedha sasa inashima kubwa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za Siasa

Serikali kuanzisha mradi wa Gridi ya maji ya Taifa

Spread the loveWaziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema katika mwaka wa fedha...

error: Content is protected !!