August 16, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Uchaguzi Z’bar wamponza mtoto wa Chacha Wangwe

Spread the love

BOB Chacha Wangwe (24), mtoto wa mwanasiasa marehemu Chacha Wangwe, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa tuhuma za kuchapisha taarifa za uongo katika mitandao ya kijamii, anaandika Faki Sosi.

Akisoma kesi hiyo namba 167, Paul Kagoshi mbele ya Waliarandwe Rema, Hakimu Mkazi katika mahakama hiyo amesema kuwa, Bob Chacha Wangwe amefikishwa mahakamani hapo kwa kutenda kosa la kuchapisha taarifa za kupotosha katika ukurasa wake Facebook.

Mshitakiwa anadaiwa kutenda hayo tarehe 15 Machi na kwamba alichapicha maneno haya “Tanzania ni ambayo….inajaza chuki wananchi … matokeo ya kubaka Demokrasia Zanzibar ni hatari zaidi ya muungano wenyewe…. Haiwezekani nchi ya Zanzibar kuwa koloni la Tanzania bara kwa sababu za kijinga.”

Mtuhumiwa amekiri kutenda makosa hayo hivyo amerudishwa rumande baada ya kukosa dhamana. Kesi hiyo itatajwa tena tarehe 17 Mei mwaka huu.

error: Content is protected !!