March 1, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Uchaguzi Z’bar wamponza mtoto wa Chacha Wangwe

Bob Chacha Wangwe (katikati) akiwasili mahakamani Kisutu

Spread the love

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuhuku kwenda jela mwaka mmoja  na nusu au kulipa faini ya Sh. 5 milioni, mtoto wa Marehemu Chacha Wangwe, Bob baada ya kukutwa na hatia kutumia vibaya mtandao, anaandika Faki Sosi.

Hukumu hiyo imetolewa leo Novemba 15, 2017 na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Huruma Shahidi ambapo alisema kuwa mtuhumiwa huyo anahatia ya kutumia vibaya mtandao wa kijamii kutokana na upotoshaji alioufanya.

Bob Wangwe alitoa maoni yake kwenye ukurasa wake wa Facebook kuhusu uchaguzi wa marudio wa Zanzibar uliofanyika Machi 20, 2016.

Kwenye kesi hiyo namba 167 ya mwaka 2016, Bob Chacha Wangwe alidaiwa kutenda kosa hilo Machi 15, 2016 kwa kuchapicha maneno haya: “Tanzania ni ambayo….inajaza chuki wananchi … matokeo ya kubaka demokrasia Zanzibar ni hatari zaidi ya Muungano wenyewe…. Haiwezekani nchi ya Zanzibar kuwa koloni la Tanzania Bara kwa sababu za kijinga.”

Wakati wa usikilizwaji wa kesi hiyo upande wa Jamhuri ulileta mahakamani hapo mashahidi sita huku upande wa utetezi shahidi alikuwa mmoja ambaye ni mshitakiwa mwenyewe.

Awali Bob alipandishwa kizimbani Mei 11, 2016 kwa tuhuma za kuchapisha taarifa za upotoshaji kwenye ukurasa wake wa wa Facebook.

error: Content is protected !!