January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Uchaguzi Zanzibar wafutwa

Spread the love

MWENYEKITI wa Tume ya Uchaguzi wa Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha ametangaza kufuta matokeo ya uchaguzi wa kisiwani humo bila kutoa sababu za kufanya hivyo. Anaandika Jabir Idrissa, Zanzibar … (endelea).

Jecha ametangaza tangazo hilo kupitia Shirika la Habari la Zanzibar (ZBC) na kuacha sintofahamu kwa wananchi wa Zanzibar wasijue nini cha kufanya.

Jecha hakuwepo katika ukumbi wa kufanya majumuisho ya kura za Urais wa Zanzibar bila kutoa taarifa yoyote.

Majukumu ya kufanya majumuisho ya kura yalikuwa yakisimamiwa na Makamo Mwenyekiti wa ZEC, Jaji Adbulhakim Issa Ameir ambaye naye alitekwa muda mchache kabla ya tangazo hilo kutolewa.

Jaji Ameir alikuwa akisimamia majumuisho hayo, lakini aliitwa nje na kuchukuliwa na askari wa FFU na kupelekwa pasipojulikana na muda mchache ujao ikatangazwa taarifa hiyo.

MwanaHALISI Online inafuatiliwa kwa karibu tukio hilo na itawaletea taarifa kamili.

error: Content is protected !!