Sunday , 5 February 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa Uchaguzi Zambia: Lungu alia rafu mpinzani wake akiongoza matokeo ya awali
Kimataifa

Uchaguzi Zambia: Lungu alia rafu mpinzani wake akiongoza matokeo ya awali

Spread the love

 

MGOMBEA upinzani nchini Zambia, Hakainde Hichilema, ameongoza katika matokeo ya awali ya uchaguzi wa urais, uliofanyika tarehe 12 Agosti 2021, dhidi ya Edgar Lungu, anayetetea kiti hicho kwa muhula wa pili. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa…(endelea ).

Kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa mapema leo Jumamosi, tarehe 14 Agosti 2021 na Tume ya Uchaguzi Zambia (ECZ), Hakainde aliyegombea kupitia Chama cha UPND, anaongoza kwa kura zaidi ya 60,000 dhidi ya Lungu.

Ambapo amepata 171,604, huku mpinzani wake wa karibu Lungu wa Chama Tawala cha Patriotic Front, akipata 110,178. Kura hizo ni matokeo ya majimbo 15 kati ya 156 ya Taifa hilo, lililoko Kusini mwa Afrika.

Wakati zoezi la kuhesabu kura likiendelea, kupitia ukurasa wake wa Twitter, Hakainde alitoa wito kwa watu wanaohesabu kura, kutenda haki wakati zoezi hilo linafanyika.

“Jua linapochomoza kwa ajili ya siku ya hatima ya Zambia, ujumbe wetu kwa wale wanaohusika na kuhesabu kura ni rahisi, haki. Haki pekee ndiyo mnayotakiwa kuifuata, ili mpate kuishi na kumiliki nchi ambayo Bwana Mungu wenu amewapa,’ ameandika Hakainde.

Wakati Hakainde akioa wito huo, Lungu kupitia ukurasa wake wa Twitter, alilalamika akidai kwamba mchakato wa uchaguzi huo haukuwa huru na wa haki.

Rais huyo wa Zambia anayemalzia muda wake, alitoa shutuma hizo baada ya mauaji ya Mwenyekiti wa chama chake katika Mkoa wa Kaskazini Magharibi, Jackson Kungo.

Lungu amedai wapinzani wake wameufanya uchaguzi huo kuwa vita, kufuatia mauaji ya Kungo.
Hii ni mara ya pili kwa miamba hao wa siasa nchini Zambia,kuchuana katika kinyang’anyiro cha urais.

Kwa mara ya kwanza, walichuana kwenye Uchaguzi Mkuu uliofanyika 2016, ambapo Lungu alitangazwa mshindi wa kiti hicho, baada ya kupata ushindi mwembamba dhidi ya Hakainde.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Papa Francis kukutana na wahanga wa vita Sudan Kusini

Spread the love  KIONGOZI wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis leo Jumamosi...

Kimataifa

Polisi ahukumiwa kifo kwa kumuua wakili

Spread the love  MAHAKAMA kuu nchini Kenya imemhukumu kifo Ofisa wa Polisi,...

Kimataifa

Hospitali za China zilifurika wagonjwa, wazee kipindi cha wa likizo ya Mwaka Mpya wa Lunar

Spread the loveHOSPITALI  nchini China zimejaa wagonjwa na wazee katika kipindi cha...

Kimataifa

Papa Francis ayataka mataifa ya nje kuacha kupora mali DRC

Spread the love  KIONGOZI wa kanisa Katoliki Papa Francis, ameyataka mataifa ya...

error: Content is protected !!