KAMATI ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) chini ya Mwenyekiti wake, Wakili Revocatus Kuuli imetangaza kuusimamisha Uchaguzi Mkuu wa klabu ya Simba kutokana na kuwepo kwa dosari mbalimbali za kikanuni za wanachama wa TFF. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).
Dosari ambazo zimejitokeza katika uchaguzi huo wa Simba ni pamoja na kutowekwa kwa matakwa ya kisheria kama kuhusisha Kamati ya Rufaa na Kamati ya Maadili huku sheria ikiwataka kutumia kanuni za uchaguzi za wanachama wa TFF.
“Ni kweli tumesimamisha mchakato huo ili wafanye maboresho, zipo dosari tumeziona kama kamati na kama wakizifanyia kazi wataendelea na uchaguzi,” amesema Kuuli.
Aidha aliongezea ya kuwa kanuni za wanachama zinataka mgombea wa nasafi ya mwenyekiti achukue fomu kwa Sh. 200,000 na nasafi nyingine ni Sh. 100,000 lakini kamati ya Simba wao wameamua kuweka kiwango cha Sh. 500,000 kwa madai kwamba wanatumia kanuni cha uchaguzi za TFF.
Uchaguzi huo ambao wagombea katika nafasi tofauti tofauti walisharudisha fomu na kuingia katika hatua ya usahiri, huku uchaguzi huo hapo awali ulipangwa kufanyika Novemba 3 mwaka huu.
Leave a comment