July 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Uchaguzi wa Meya Dodoma, Chadema, CCM nusura wazichapa kavukavu

Spread the love

UCHAGUZI wa kuwachagua Meya na Naibu Meya katika Manispaa ya Dodoma jana uligubikwa na vurugu baada ya wanaodaiwa kuwa makada wa chama cha Mapinduzi na wale wa Chadema kutaka kuzichapa kavukavu nje ya ukumbi wa manispaa hiyo. Anaandika Dany Tibason, Dodoma … (endelea).

Hali hiyo ambalo lilitokea wakati wa kuwaapisha Madiwani 56 pamoja na kuwachagua Naibu Meya na Meya wa Manispaa ya Dodoma lilofanyika katika viwanja hivyo.

Tukio hilo ambalo lilivikutanisha vyama vya   Chadema na CCM katika viwanja hivyo ambapo wanaodaiwa kuwa Makada na wapenzi wa CCM waliokuwa wamevaa sare za chama hicho walianza kuimba nyimbo za kuwakashifu Chadema.

Mara baada ya kuona wanakashifiwa wanaodaiwa kuwa Makada na wapenzi wa Chadema na wao walijibu mapigo na kuwakashifu CCM hali ambayo ilisababisha kutokea kwa vurugu kubwa.

Vurugu hizi zilidumu kwa takribani dakika 20 mbapo walijikuta viongozi wa vyama hivyo akiwemo Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya yaDodoma, Aifraim Kolimba (CCM) na Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Dodoma, Vicent Imanuel kuamua kuzichapa kavukavu.

Viongozi hao walikunjana kwa dakika kadhaa mpaka pale alipotokea Mgambo wa Manispaa na kuweza kuwatuliza.

Mara baada ya kuonekana tukio hilo limetulia makada hao walianza kurushiana matusi ya nguoni huku kila mmoja akikikashifu chama cha mwenzake.

Tukio hilo lilikoma mara baada ya Diwani wa Kata ya Kizota (Chadema) Jamal Yaled ambaye alikuwa mgombea wa nafasi ya Naibu Meya alipowataka makada na viongozi wa Chama chake kutulia.

‘’Jamani wala msipigane, hawa tutawanyoosha katika Baraza nawaomba mtulie,’’ amesema Yaled huku akishangiliwa.

Ndipo wanachama hao walipotulia na mara baada ya muda Askari wa FFU waliingia katika viwanja hivyo na kutuliza hali ya vurugu iliyokuwepo awali.

Katika uchaguzi huo Madiwani 48 kati ya 56 walimpitisha Japhary Mwanyemba kuwa Meya wa Manispaa hiyo kwa asilimia 82.

Akitangaza matokeo hayo,Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Clemence Mkusa alisema Naibu Meya alikuwa Jumanne Ngede.

‘’Namtangaza kwenu Jumanne Ngede kuwa Naibu Meya ya Manispaa ya Dodoma kwa kura 48 kwa asilimia 82 kama za Mwanyembam,’’ amesema.

Akizungumza mara baada ya kuchaguliwa Mwanyemba aliwataka madiwani hao kuvunja makundi kwa kuhakikisha wanatetea matatizo ya Wananchi kwa kuwaletea maendeleo.

error: Content is protected !!