Thursday , 28 March 2024
Home Gazeti Habari Uchaguzi TLS: Wagombea urais wamwaga sera zao
Habari

Uchaguzi TLS: Wagombea urais wamwaga sera zao

Wagombea Urais TLS wakiwa kwenye mdahalo
Spread the love

 

WAGOMBEA Urais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), wamechuana vikali katika kueleza sera zao, ili kuwashawishi wapiga kura kuwachagua. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Wagombea hao watano, kwenye uchaguzi huo utakaofanyika tarehe 15 Aprili 2021 ni; Flaviana Charles, Shehzada Walli, Albert Msando, Francis Stolla na Dk. Edward Hoseah.

Leo Jumanne, tarehe 6 Aprili 2021, wagombea hao wamechuana vikali kwenye mdahalo ulioandaliwa na TLS ili kuwawezesha kueleza sera zao na walivyojipanga kuwaongoza kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Miongoni mwa masuala yaliyojadiliwa katika mjadala huo, ni ukusanyaji mapato ya TLS na kudhibiti matumizi yake, uboreshaji masilahi ya wanachama wake, kudhibiti mawakili vishoka pamoja na uimarishwaji wa mahusiano baina ya chama hicho na Serikali.

Mawakili hao wameingia katika uchaguzi huo, kutafuta nafasi ya kumrithi Dk. Rugemeleza Nshalla, anayemaliza muda wake.

Akijinadi katika mjadala huo, Flaviana amesema, akishinda uchaguzi huo, ataibua fursa za uwekezaji kwa kutumia rasilimali za TLS, ili kuboresha mapato ya chama hicho na kuwainua kiuchumi wanachama wake.

Albert Msando, mgombea Urais TLS

“Moja kabisa, TLS kuwa na pesa yake yenyewe, miaka yote tumekuwa tukitegemea michango ya wanachama na imekuwa ikiwaelemea wanachama, maisha yetu yanategemea michango ya wanachama na kazi zetu zinatutegemea,” amesema Flaviana na kuongeza:

“Katika uongozi wangu, tutakutana na wadau mbalimbali watatatua changamoto zetu, naamini tukiwa na pesa matatizo yote yatatulika, tunaweza kufanya mambo makubwa kwa members (wanachama) wetu, natamani kuona TLS inatoka sehemu moja kwenda nyingine, kuondoa changamoto za wanasheria.”

Kwa upande wake Msando, amesema akichaguliwa ataboresha utendaji wa TLS, kwa kuondoa mapungufu yaliyopo, kuongeza vyanzo vya mapato na kudhibiti mapato na matumizi.

Shehzada Walli mgombea Urais TLS

“Nitaona namna gani tunaenda na mapungufu yaliyopo, mapungufu mengi yapo ambapo mpango mkakati wetu unaonesha asilimia 57 hawaridhiki na utendaji, inaonesha kama kuna tatizo. Lazima atoke mtu ambaye ataweza kulitatua pamoja na wanachama husika,” ameahidi Msando na kuongeza:

“Kabla ya kuongeza vyanzo vya mapato lazima tuangalie tunaweza kupunguza vipi matumizi yetu ili chama kisiwe na utegemezi. Mimi naona tufike mahali tuwe na chama kinachoweza dhibiti mapato yake yanayopatikana, hizi ni fedha za wanachama lazima tuzisimamie,” amesema

Naye Stolla aliyewahi kuwa rais wa TLS amesema, ataboresha mifumo ya TLS ikiwemo kuunda kamati maalumu itakayokusanya maoni ya wanachama, juu ya namna ya kuboresha masilahi yao ndani ya chama hicho.

“Nitafanya maboresho ya taasisi na mifumo ndani ya chama, nafahamu TLS kiliundwa kwa sheria, chama kupitia ngazi mbalimbli kina mamlaka ya kuweka kamati kusaidia kufanya kazi, miongozini mwa kamati tutakazoziunda ni kamati ya kutafuta maoni ya wanachama kuhusu maboresho ya namna gani ya kulinda maslahi yao,” ameahidi Stolla.

Kwa upande wake, Dk. Hoseah ameahidi kumaliza changamoto ya mawakili vishoka, ili kulinda maslahi ya mawakili.

“Nitaanzisha encrypted advocate, ili kuondoa vishoka. Vishoka hawatatumia mihuri ya mawakili ili kuwaondoa,” amesema Dk. Hoseah, aliyewahi kuwa mkurugenzi mkuu wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (Takukuru).

Aidha, Dk. Hoseah ameahidi kuboresha mahusiano ya chama hicho na Serikali kwa kuanzisha majadiliano ili kuangalia namna ya kurejesha mahusiano mazuri baina yao, kama ilivyokuwa zamani.

Dk Edward Hoseah mgombea Urais TLS

“Jambo lingine ni suala la mahusiano yetu na mahakama, nikiwa kiongozi nitajenga mahusiano mazuri kati ya wanasheria na mahakama. Kwa maana kwamba tunahitaji mjadala na mahakama, huko nyuma ilikuwepo nataka niifufue ili tuwe vizuri na mahakama,” amesema Dk. Hoseah.

Mgombea mwingine, Walli amesema, katika uongozi wake ataanzisha kampeni ya kuelimisha jamii, juu ya umuhimu wa kuchangia huduma za msaada wa kisheria, zinazotolewa na mawakili ili wajipatie kipato.

“Sisi kama mawakili, tunatoa huduma zetu nyingi bure, watu wanakuja kuchukua ushauri wanaondoka. Lakini madaktari wanapata hela wanapotoa ushauri. Tuanze kampeni kuiambia jamii mawakili walipwe kwa muda wao,” amesema Walli.

Akitaja sera zake, Walli amesema ataunda taasisi ya usuluhishi ndani ya TLS, ambayo itasaidia kuongez amapato ya chama hicho, na kuondoa mzigo wa michango kwa wanachama wake.

Francis Stolla mgombea Urais TLS

“Ni muhimu kuangalia kwenye uwekezaji wa chama, kwenye mpango mkakati wetu kuna taasisi ya kuleta usuluhishi. Tukifanikisha kwa mwaka huu itatuletea mapato, watu watakuja kwetu kusuluhisha lakini mawakili wetu tutawafudisha watasuluhisha na kupata hela,” amesema Walli.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

HabariSiasa

Dk. Rose Rwakatare atoa kadi 500 kila Wilaya Morogoro

Spread the loveMWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Morogoro, Dk...

ElimuHabari

CBE, WMA wasaini makubaliano wanafunzi kusoma wakifanyakazi

Spread the loveNAIBU Spika Musa Azzan Zungu amekipongeza Chuo cha Elimu ya...

HabariTangulizi

Dk. Slaa, Mwabukusi kuhojiwa na jeshi la Polisi Mbeya

Spread the loveJESHI la Polisi jijini Mbeya, linawashikilia kwa mahojiano Dk. Wilbroad...

HabariHabari Mchanganyiko

Kairuki Hospital Green IVF  yawanoa madaktari kuhusu upandikizaji mimba

Spread the love KITUO cha Upandikizaji Mimba cha Kairuki Hospital Green IVF...

error: Content is protected !!