Wednesday , 8 February 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa Uchaguzi Spika Bunge Marekani bado ngoma ngumu
Kimataifa

Uchaguzi Spika Bunge Marekani bado ngoma ngumu

Spread the love

Mrepublican Kevin McCarthy wa California ameshindwa katika duru ya nne, ya tano na ya sita ya uchaguzi wa kuwa spika wa Baraza la Wawakilishi nchini Marekani. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa…(endelea).

Hii ni baada ya idadi ya kutosha ya Warepublican kupiga kura ya uteuzi wa kushangaza wa Byron Donalds katika siku ya pili ya jaribio la bunge kumchagua spika.

McCarthy amekuwa akisaka uspika, lakini alishindwa mara tatu katika upigaji kura wa Jumanne katika jitihada ya kusaka kura 218 katika baraza lenye wajumbe 435, na alishindwa katika duru tatu nyingine za upigaji kura jana Jumatano.

Katika duru ya nne, tano na sita ya upigaji kura, takwimu zilibakia pale pale huku McCarthy akipata kura 201, Warepublican 20 wakampigia kura Donalds, naye mjumbe wa Indiana Victoria Spartz akipiga kura ya ‘kuwepo’ yaani kumaanisha yupo bungeni lakini hatopiga kura ya kuunga mkono au kupinga.

Chama cha Republicana ambacho kilichukua udhibiti wa Baraza la Wawakilishi Novemba, awali kilishindwa kufikia muafaka wa kumuunga mkono McCarthy kufuatia duru tatu za upigaji kura jana.

McCarthy hata hivyo ameapa kumaliza mapambano hayo na kupata wadhifa wa spika. Bunge liliahirisha vikao hadi leo mchana.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Tetemeko la ardhi Uturuki: Vifo vyaongezeka hadi 4,800

Spread the love  Idadi ya vifo vilivyotokana na tetemeko lililotokea jana Jumatatu...

Kimataifa

Tetemeko la ardhi laua watu 300 Uturuki, Syria

Spread the love  WATU  300 wamefariki dunia katika tetemeko kubwa la ardhi...

Kimataifa

Urusi, Ukraine zabadilishana wafungwa wa kivita

Spread the loveJUMLA ya wafungwa 179 wa kivita wa Urusi na Ukraine...

Kimataifa

Papa Francis kukutana na wahanga wa vita Sudan Kusini

Spread the love  KIONGOZI wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis leo Jumamosi...

error: Content is protected !!