Saturday , 2 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Uchaguzi Serikali za Mitaa: Malalamiko kila kona
Habari za SiasaTangulizi

Uchaguzi Serikali za Mitaa: Malalamiko kila kona

Sanduku la kura
Spread the love

KIPYENGA cha uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji, kimepulizwa nchini kote, huku malalamiko lukuki yakiripotiwa kutoka katika baadhi ya maeneo. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Uchaguzi katika ngazi hizo, umepangwa kufanyika tarehe 24 Novemba mwaka huu, huku kampeni zikitarajiwa kuanza tarehe kuanzia 17 hadi 23 Novemba.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Suleman Jafo amesema, matatizo yaliyopo, ni madogo kulinganisha na ukubwa wa nchi.

Katika jimbo la Mbozi, mkoani Songwe, kumeripotiwa kuwapo kwa hujuma kadhaa, ikiwamo wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi kukimbia ofisi zao.

Mbunge wa Mbozi Pascal Haonga,amedai kuwa baadhi ya wasimamizi, wamezima simu zao na wengine wamegoma kupokea.

Anasema, “mikakati mibaya imepangwa kuihujumu Chadema katika jimbo hili. Kuna baadhi ya vijiji wasimamizi wasaidizi wamefika vituoni, lakini wanadai kuwa fomu za wagombea wetu, tayari zimechukuliwa.”

Mbunge huyo anasema, hatua ya wasimamizi hao kutopatikana kwenye simu, kunalifanya zoezi zima la uchukuaji fomu kwa wagombea wa upinzani kuwa mgumu.

Mkoani Kilimanjaro, kumeripotiwa hujuma katika wilaya ya Moshi Vijijini, Rombo, Hai, Siha na Moshi Mjini.

Katika jimbo la Vunjo, imeelezwa kuwa hali si nzuri kwa wagombea wa upinzani, kufuatia kukumbana na vikwazo kadhaa, ikiwamo kunyimwa fomu kwa ajili ya wagombea wake.

Katika jimbo la Karatu, mkoani Manyara, baadhi ya wasimamizi wa uchaguzi, wameamua kufunga ofisi na kutokomea kusikojulikana.

“Hata wale wasimamizi waliopo vituoni, wanasema hawajaletewa fomu. Wengine wanasema, fomu wanazo ila hawana mihuri,” ameeleza mmoja wa wagombea wa nafasi ya uenyekiti Karatu Mjini.

Mbunge wa Tarime Mjini (Chadema), Esther Matiko, ameeleza kuwa katika jimbo lake, kumebadirishwa vituo vya uchukuaji wa fomu. Anasema, kufuatia hali hiyo, chama chake kiliamua kuwaandikia barua wasimamizi wa uchaguzi, ili kujua zilipo ofisi zao.

“Kwangu, baada ya kuwaandikia, jana walionyesha ofisi. Lakini nimesikia katika jimbo la Tarime Vijijini, “kuna hujuma za kukosekana fomu kwa ajili ya wagombea wetu.”

Kutoka wilayani Kishapu, mkoani Shinyanga, wagombea wa Chadema, katika kijiji cha Mwataga kata ya Mwataga, wamevamiwa na askari wa Mgambo na kunyang’anywa fomu za serikali walizokuwa wamekabidhiwa.

Mgombea mmoja wa kitongoji amejeruhiwa kichwani na amekimbizwa hospitali. 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Mwalimu jela miaka mitatu kwa rushwa

Spread the loveMAHAKAMA ya Hakimu Mfawidhi, wilaya ya Igunga, mkoani Tabora imemhukumu...

Habari za Siasa

Rais Samia kuzindua programu ya nishati safi ya kupikia kwa wanawake Afrika

Spread the loveRais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuzindua programu ya...

Habari za Siasa

AG aiagiza kamati ya maadili kuwashughulikia mawakili wanaokiuka maadili

Spread the loveMWANASHERIA Mkuu wa Serikali (AG), Dk. Eliezer Feleshi, ameagiza Kamati...

Habari za Siasa

Jaji avunja ukimya sakata la Mpoki kusimamishwa uwakili

Spread the loveJAJI Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Juma, amekitaka Chama cha...

error: Content is protected !!