Thursday , 30 March 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Uchaguzi Muhambwe, Buhigwe: CCM, ACT-Wazalendo hapatoshi
Habari Mchanganyiko

Uchaguzi Muhambwe, Buhigwe: CCM, ACT-Wazalendo hapatoshi

Zitto Kabwe kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo
Spread the love

 

IKIWA imesalia siku moja kwa chaguzi ndogo katika Jimbo la Buhigwe na Muhambwe, mkoani Kigoma kufanyika, Chama cha ACT-Wazalendo na Chama Cha Mapinduzi (CCM), vinatoana jasho kusaka kura za ushindi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Katika chaguzi hizo ndogo, zinazotarajiwa kufanyika kesho Jumapili tarehe 16 Mei 2021, hadi sasa vyama hivyo vinaonekana kuchuana vikali, ambapo CCM kinapambana kutetea majimbo hayo huku ACT-Wazalendo, kikitafuta nafasi ya kupata wawakilishi wake bungeni.

Wagombea katika Jimbo la Muhambwe ni Dk. Florence Samizi (CCM) na Julius Masabo (ACT-Wazalendo). Na Buhigwe wanaogombea ni, Galula Kudra (ACT-Wazalendo) na Mwalimu Eliadory Kavejuru (CCM) .

Mbali na kutumia majukwaa ya kampeni, vita hiyo ya kusaka ushindi imeshika kasi mitandaoni, baada ya ACT-Wazalendo kuhoji kwa nini CCM imetumia viongozi wa kiserikali, kufanya kampeni kwenye chaguzi hizo.

Hoja hiyo iliibuliwa jana tarehe 14 Mei 2021, na Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, aliyesema licha ya CCM kuelekeza nguvu kubwa katika chaguzi hizo, chama chake kitashinda.

“Muhambwe na Buhigwe ACTwazalendo inapambana dhidi ya Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Mawaziri 9, Wabunge wa CCM 39 na kina Lazaro Nyalandu. Hata hivyo tutawachapa. Masabo atashinda Muhambwe, Garula atashinda Buhigwe,” aliandika Zitto Twitter.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, aliongoza kampeni za chaguzi hizo tarehe 4 hadi 5 mwaka huu, huku Makamu wa Rais, Dk. Phillip Mpango, akitarajiwa kufunga kampeni hizo, leo tarehe 15 Mei 2021.

Akijibu hoja hiyo, Mbunge wa Mtama (CCM), Nape Nnauye, kupitia ukurasa wake wa Twitter, amesema chama hicho hakina jambo dogo, ndiyo maana kimeelekeza nguvu yake katika chaguzi hizo.

“Hawa ni viongozi wa CCM, CCM hatuna jambo dogo, kwa nini utupangie nani aje, nani asije?” amehoji Nape.

Mwanasiasa huyo ambaye ni miongoni mwa wabunge wa CCM wanaoshiriki kampeni hizo amesema “Uchaguzi ni hesabu sio porojo. Wapiga kura Muhambwe waliojiandikisha ni 127766, WanaCCM wako 69,421. Hata wakipiga wana CCM peke yake Samizi kashinda! Kila mwanaCCM akitafuta kura moja tu. Done.”

Baada ya Nape kuandika hayo, Mgombea wa ACT-Wazalendo Muhambwe, Masabo amemueleza mwanasiasa huyo kwamba hawatashinda katika jimbo hilo.

“Kaka Salaam! Hao Wana CCM hawakupiga Kura kwenye last year General Election? Maana The Late (Hayati Nditiye), mgombea wenu hakupata hata nusu ya kura za Wwanachama wenu wote wa Muhambwe. Nasikia Umekuja Kumchukua Mgombea wenu, hapa Muhambwe utaondoka mwenyewe kama Ulivyokuja,” ameandika Masabo.

ACT-Wazalendo kiimepanga kufunga kampeni hizo kwa kufanya mikutano sita kwa kila jimbo, huku Zitto, akitarajiwa kurusha kete ya mwisho Muhambwe wakati Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Zanzibar, Juma Duni Haji akifunga Buhigwe.

Awali, viongozi hao wa ACT-Wazalendo walipanga kufanya mikutano katika majimbo yote, lakini ratiba hiyo imeahirishwa baada ya chopa (Helkopta), waliyopanga kutumia kupata hitilafu.

Chaguzi hizo ndogo zimeitishwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), baada ya aliyekuwa Mbunge wa Muhambwe, Atashatsta Nditiye, kufariki dunia, na aliyekuwa Mbunge wa Buhigwe, Dk. Mpango, kuteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan, kuwa Makamu wa Rais wa Tanzania.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

NMB Bonge la Mpango – ‘Moto Uleule’ yazinduliwa, Milioni 180…

Spread the loveMSIMU wa tatu wa Kampeni ya kuhamasisha utamaduni wa Kuweka...

Habari Mchanganyiko

Rais Samia awataka wahariri kufanya kazi bila uoga, upendeleo

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan amewataka wahariri wa vyombo...

Habari Mchanganyiko

STAMICO yasaini mkataba wa bilioni 55.2 kuchoronga miamba GGML

Spread the loveSHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO) limezidi kufanya vizuri katika...

Habari Mchanganyiko

NMB yatoa traksuti za Mwenge wa Uhuru Mtwara

Spread the loveBENKI ya NMB imetoa traksuti kwa mkoa wa Mtwara ambako...

error: Content is protected !!