Thursday , 25 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Uchaguzi Mkuu: ‘Waandishi wasibague’ – THRDC
Habari Mchanganyiko

Uchaguzi Mkuu: ‘Waandishi wasibague’ – THRDC

Onesmo Olengurumwa, Mratibu wa Kituo cha Watetezi wa Haki za Binadamu Taifa
Spread the love

WAANDISHI wa habari nchini, wametakiwa kutoripoti habari kwa ubaguzi, katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).

Akichangia kwenye mjadala ulioendeshwa kwa njia ya mtandao na kuongozwa na Deus Kibamba, Mkurugenzi wa Kituo cha Taarifa kwa Wananchi (TCIB), Onesmo Olengurumwa Mratibu wa THRDC amesema, wanahabari hawatakiwi kuegemea upande wowote wa siasa.

Baadhi ya waalikwa kwenye mdahalo huo ni pamoja na yenyewe THRDC; Nevile Meena, Katibu wa Jukwaa la Katiba (TEF); Edwin Soko, Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mwanza (MPC); David Mbulumi, Meneja wa Program wa Baraza la Vyombo vya Habari nchini (MCT); Salim Said, Mwakilishi wa Chama cha Wanahabari Wanawake (TAMWA) na kuongozwa na Kibamba kutoka TCIB.

“Waandishi hamtakiwa kuegemea upande wowote wa kisiasa, tuwape nafasi watu wenye kuweka mbele maslahi ya Taifa,” amesema.

Amesema, THRDC itahakikisha inatoa elimu kwa wanahabari na kuwahimiza kuzingatia uweledi wao.

Sanduku la kura

Katibu wa TEF, Meena amesema wanahabari bado wapo kwenye mazingira magumu ya kufanya kazi, na kwamba hawewezi kukosa upande kwasababu ya kuwepo kwa utashi binafsi.

Amewataka wanhabari kuwa makini na mazingira ya sasa ya kisiasa “tujifunze kuogelea kwenye mto wenye mamba bila kuliwa.”

Soko wa MPC amesema, kuwa klabu yake itatoa mafunzo kwa wanahabari juu ya namna ya kushiriki kwenye kampeni za uchaguzi kwa uweledi.

1 Comment

  • Wanahabari wa TSN, TBC, ZBC, Zanzibar Leo, Uhuru,Channel Ten nk wasipoegemea upande mmoja watapata wapi mkate wao wa kila siku? Wameajiriwa kupendelea

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

THRDC yaongeza mkataba wa ushirikiano na ABA

Spread the love  MTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC),...

Habari Mchanganyiko

Rufaa ya Equity Benki, State Oil yakwama

Spread the loveMAHAKAMA ya Rufani, jijini Dar es Salaam, imeshindwa kuendelea na...

Habari Mchanganyiko

Bodaboda waeleza mafanikio mafunzo usalama barabarani

Spread the loveMADEREVA bodaboda katika Jiji la Dodoma wameeleza jinsi mafunzo ya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yaahidi kuendelea kuunga mkono Serikali za Mitaa

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imesisitiza dhamira yake ya...

error: Content is protected !!