September 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Uchaguzi Mkuu Tanzania Jumatano Oktoba 28

Mwenyekiti wa NEC, Semistocles Kaijage

Spread the love

TUME ya Taifa ya Uchaguzi  (NEC) nchini Tanzania imesema, Uchaguzi Mkuu wa udiwani, ubunge na Urais wa Tanzania utafanyika Jumatano Oktoba 28, 2020. Anaripoti Hamis Mguta, Dar es Salaam … (endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Jumanne tarehe 21 Julai 2020, Mwenyekiti wa NEC, Semistocles Kaijage amesema uteuzi wa wagombea itakuwa Agosti 25,2020 na kampeni zitaanza Agosti 26 hadi Oktoba 27,2020.

Hii itakuwa mara ya kwanza Uchaguzi Mkuu unafanyika katikati ya wiki yaani Jumatano tofauti na chaguzi zilizopita ambazo zilikwua zikifanyika Jumapili.

Endelea kufuatilia MwanaHALISI Online na MwanaHALISI TV

error: Content is protected !!