UCHAGUZI Mkuu Nchini Kenya upo mashakani kufanyika Oktoba 26 kama ilivyotangazwa na Tume ya Uchaguzi na Mipaka ya nchi hiyo, (IEBC), baada ya wapigakura kufungua kesi katika mahakama ya juu wakitaka uchaguzi usifanyike, anaandika Mwandishi wetu.
Leo kesi hiyo imeunguruma katika mahakama hiyo na kuahirishwa mpaka kesho asubuhi yatakapotolewa maamuzi kama uchaguzi huo utafanyika kama ulivyopangwa au la.
Mahakama ya juu nchini humo ilifuta uchaguzi mkuu na hivyo IEBC kutangaza Oktoba 26 kuwa siku ya Wakenya kushiriki katika uchaguzi wa marudio.
Wakati hayo yakiendelea nchini humo, mpinzani mkuu nchini humo, Raila Odinga ametangaza kujitoa katika uchaguzi huo kwa madai kuwa IEBC imeshindwa kutekeleza maagizo ya mahakama ya juu.
Hata hivyo, Rais Uhuru Kenyatta yeye amesisitiza kwamba lazima uchaguzi huo wa marudio ufanyike kama ulivyopangwa nchini humo na kwamba kila kitu kinaenda vizuri.
Leave a comment