Friday , 1 March 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Uchaguzi Mkuu DR Congo sasa 2018
Kimataifa

Uchaguzi Mkuu DR Congo sasa 2018

Rais wa DR Congo, Joseph Kabila (kushoto). Picha ndogo ni mpinzani wake, Moise Katumbi
Spread the love

TUME ya Uchaguzi Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), imetangaza kwamba uchaguzi mkuu nchini humo sasa utafanyika Desemba 2018.

Hata hivyo, upinzani haujafurahishwa na hatua hiyo ambao umetaka Rais Joseph Kabila aondoke madarakani kwa sasa.

Awali uchaguzi huo ulipangwa kufanyika mwaka huu chini ya makubaliano yaliyoafikiwa mwaka jana, lakini tume ya uchaguzi imechelewa kuuandaa.

Lakini sasa tume hiyo imetangaza kwamba uchaguzi wa rais, wabunge na viongozi wa serikali za majimbo utafanyika mnamo 23 Desemba, 2018.

Upinzani umepinga tarehe hiyo na kusema haikubaliki huku ukisisitiza kwamba kwamba ni sharti Rais Kabila aonondoke madarakani kufikia mwisho wa mwaka huu.

“Tunaikataa kalenda iliyotolewa ya uchaguzi…tunachokitaka kwa sasa hivi ni Kabila kuondoka madarakani kufikia 31 Desemba, 2017,” alisema Augustin Kabuya, msemaji wa chama kikuu cha upinzani cha Union for Democracy and Social Progress (UDPS).

Ofisa wa tume ya uchaguzi, Jean-Pierre Kalamba amesema matokeo ya awali katika uchaguzi huo yatatangazwa katika kipindi cha wiki moja baada ya upigaji kura kufanyika, mnamo tarehe 30 Desemba, lakini matokeo kamili yatatangazwa tarehe 9 januari, 2019.

Rais mpya anatarajiwa kuapishwa 12 Januari, 2019. Kiongozi wa upinzani Moise Katumbi amepuuza mpango huo tume ya uchaguzi .

“Utawala huu dhalimu unataka kuendeleza ukosefu wa uthabiti na dhiki dhidi ya wananchi,” Katumbi amesema.

“Hatutakubali kalenda hii. Kabila sharti aondoke,” aliandika kwenye Twitter.

Hali ya wasiwasi imekuwepo nchini humo tangu Kabila alipokataa kuondoka madarakani mwishoni mwa mwaka jana baada ya kumalizika kwa muhula wake wa pili na wa mwisho.

Tume ya uchaguzi imesema moja ya sababu iliyosababisha kushindwa kuandaa uchaguzu kwa wakati ni kutokana na matatizo ya kuandaa sajili ya wapiga kura, hasa eneo lenye misukosuko la Kasai katikati mwa nchi hiyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Wanajeshi Ukraine waishiwa risasi, 31,000 wauawa

Spread the loveRais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy amesema zaidi ya wanajeshi 31,000...

Kimataifa

Waziri mkuu Palestina ajiuzulu

Spread the loveWaziri Mkuu wa Palestina, Mohammed Shtayyeh ametangaza kujiuzulu pamoja na...

Kimataifa

Rais mstaafu ahukumiwa miaka 4 jela

Spread the loveMahakama ya mjini Tunis imemhukumu rais wa zamani wa Tunisia,...

Kimataifa

Malawi yaondoa vikwazo vya viza kwa nchi 79 ikiwamo TZ

Spread the loveWaziri wa usalama wa ndani nchini Malawi, Ken Zikhałe ametangaza...

error: Content is protected !!